Matendo 14
14
Paulo na Barnaba wakiwa Ikonio
1Ikawa huko Ikonio wakaingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi; na kwa vile walivyonena, kundi kubwa la Wayahudi na la Wagiriki wakaamini. 2#Mdo 13:45 Lakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa Mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.
3 #
Mdo 19:11; Mk 16:20; Ebr 2:4 Basi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa ushujaa katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao. 4Lakini jamii ya watu wa mjini wakafarakana; hawa walikuwa upande wa Wayahudi, na hawa upande wa mitume. 5#Mdo 14:19; 2 Tim 3:11 Hata palipotokea shambulio la watu wa Mataifa na Wayahudi pamoja na wakubwa wao juu yao, kuwatenda jeuri na kuwapiga kwa mawe, 6#Mt 10:23 wao wakapata habari wakakimbilia Listra na Derbe, miji ya Likaonia, na nchi zilizo kandokando; 7#Mdo 11:19,20 wakakaa huko, wakiihubiri Injili.
Paulo na Barnaba wakiwa Listra na Derbe
8 #
Mdo 3:2; 9:33; Yn 9:1 Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja, asiyeweza kutumia miguu yake na aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa kwake. 9#Mdo 3:4; Mt 9:28 Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; naye Paulo akamkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa, 10akasema kwa sauti kuu, Simama kwa miguu yako sawasawa. Akasimama upesi akaenda. 11#Mdo 28:6 Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa lugha ya Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu. 12Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji. 13Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ng'ombe na mataji ya maua hadi malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na umati wa watu.
14Lakini mitume Barnaba na Paulo, walipopata habari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika umati wa watu, wakipiga kelele, 15#Kut 20:11; Zab 146:6; Isa 37:16; Yer 32:17; Yak 5:17 wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; tunawahubiria Habari Njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; 16#Mdo 17:30 ambaye zamani zilizopita aliwaacha mataifa yote waende katika njia zao wenyewe. 17#Zab 147:8; Yer 5:24 Lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema, akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha. 18Na kwa maneno hayo wakawazuia watu kwa shida, wasiwatolee dhabihu.
19 #
2 Kor 11:25; 2 Tim 3:11 Lakini Wayahudi wakafika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hata wakampiga kwa mawe Paulo, wakamburuta nje ya mji, wakidhania ya kuwa amekwisha kufa. 20Lakini wanafunzi walipokuwa wakimzunguka pande zote, akasimama, akaingia ndani ya mji; na kesho yake akatoka, akaenda zake pamoja na Barnaba mpaka Derbe.
Paulo na Barnaba warudi Antiokia ya Shamu
21 #
Mt 28:19
Hata walipokwisha kuihubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, 22#Mdo 11:23; 1 The 3:3; Mt 7:14 wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwahimiza wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi. 23#Mdo 13:3 Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini. 24Wakapita kati ya Pisidia wakaingia Pamfilia. 25Na baada ya kuhubiri lile neno katika Perge wakateremka mpaka Atalia.
26 #
Mdo 13:1,2 Na kutoka huko wakaabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza. 27#1 Kor 16:9; Mdo 11:18 Hata walipofika wakalikutanisha kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwamba amewafungulia Mataifa mlango wa imani. 28Wakaketi huko wakati usiokuwa mchache, pamoja na wanafunzi.
Currently Selected:
Matendo 14: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.