Kumbukumbu la Torati 31
31
Yoshua achukua mahali pa Musa
1Musa akaenda akawaambia Waisraeli maneno haya yote. 2#Hes 20:12; 27:13; Kut 7:7; Kum 34:7; Hes 27:17; 1 Fal 3:7; Kum 3:27 Akawaambia, Mimi leo ni mwenye miaka mia moja na ishirini; siwezi tena kutoka na kuingia, na BWANA ameniambia, Hutavuka mto huu Yordani. 3#Kum 9:3 BWANA Mungu wako, ndiye atakayevuka mbele yako, atawaangamiza mataifa haya mbele yako, nawe utawamiliki; na Yoshua atavuka mbele yako, kama BWANA alivyonena. 4#Hes 21:21-35 Na BWANA atawatenda hao kama vile alivyowatenda Sihoni na Ogu, wafalme wa Waamori, na nchi yao, ambao aliwaharibu. 5#Kum 7:2 Naye BWANA atawatia mikononi mwenu, nanyi mtawatenda kadiri ya amri ile niliyowaamuru. 6#Yos 10:25; 1 Nya 22:13; Kum 1:29; 7:18; 20:4; Zab 118:6; Yos 1:5; Ebr 13:5 Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana BWANA, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha. 7#Kum 1:38; 3:28 Musa akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote, Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi BWANA aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha. 8#Yos 1:5; Ebr 13:5; Kut 13:21; 33:14; Zab 37:3; Rum 8:31; 1 Nya 28:20 Naye BWANA, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.
Kusomwa kwa torati kila baada ya miaka saba
9 #
Kum 17:18; Hes 4:15; Yos 3:3; 1 Nya 15:12 Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, wana wa Lawi, waliolichukua sanduku la Agano la BWANA, na wazee wote wa Israeli. 10#Kum 15:1; 16:13-15; Law 23:34 Musa, akawaamuru, akasema, Mwisho wa kila mwaka wa saba, wakati wa maachilio, wakati ulioamriwa wa sikukuu ya vibanda, 11#Kum 16:16; Yos 8:34; 2 Fal 23:2; Neh 8:1 Israeli wote wafikapo ili kuonekana mbele za BWANA, Mungu wako, mahali pale atakapopachagua, uisome torati hii mbele ya Israeli wote masikioni mwao. 12#Kum 4:10 Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto, na mgeni wako aliyemo malangoni mwako wapate kusikia na kujifunza, na kumcha BWANA, Mungu wenu, na kuangalia kutenda maneno yote ya torati hii; 13#Kum 11:2; Mit 22:6; Efe 6:4; Zab 78:6,7 na watoto wao wasiojua, wapate kusikia na kujifunza kumcha BWANA, Mungu wenu, siku zote mtakazokaa katika nchi mnayoivukia Yordani ili kuimiliki.
Maagizo ya Mungu kwa Yoshua na Musa
14 #
Hes 27:13
BWANA akamwambia Musa, Tazama, siku zako za kufa zinakaribia, umwite Yoshua, nanyi mkajihudhurishe katika hema ya kukutania, ili nipate kumwagiza kazi. Musa na Yoshua wakaenda, wakajihudhurisha ndani ya hema ya kukutania. 15#Kut 33:9; Zab 99:7 BWANA akaonekana katika Hema katika nguzo ya wingu; na ile nguzo ya wingu ikasimama juu ya mlango wa Hema. 16#2 Sam 7:12; Kut 32:6; 34:15; Amu 2:17; 10:6,13; Kum 32:15; 1 Fal 11:31-33; 2 Fal 22:16,17; Isa 1:4; Yer 2:13; 17:3 BWANA akamwambia Musa, Angalia, wewe utalala na baba zako; na watu hawa wataondoka, wataifuata kwa ukahaba miungu ya kigeni ya nchi waiendeayo kuwa kati yao, nao wataniacha mimi na kulivunja agano langu, nililofanya nao. 17#2 Nya 15:2; 24:20; Kum 32:20; Zab 104:29; Isa 8:17; 64:7; Eze 39:23; Hes 14:42; Amu 6:13; Isa 63:17 Ndipo hasira yangu itakapowaka juu yao siku hiyo, nami nitawaacha, nitawaficha uso wangu, nao wataliwa, tena watajiliwa na mambo maovu mengi na mashaka; hata waseme siku hiyo, Je! Kujiliwa kwetu na maovu haya si kwa sababu Mungu wetu hayumo kati yetu? 18Nami nitawaficha uso wangu kwa kweli siku hiyo, kwa maovu yote waliyoyafanya, kwa kuigeukia hiyo miungu mingine. 19Basi sasa jiandikieni wimbo huu, uwafundishe wana wa Israeli; kawatie vinywani mwao, ili uwe shahidi kwangu wimbo huu, juu ya wana wa Israeli. 20#Kum 32:15; Neh 9:26; Zab 17:10; 73:7; Yer 5:28; 50:11; Hos 13:6 Kwa kuwa nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao, imiminikayo maziwa na asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu. 21#1 Nya 28:9; Hos 5:3; 13:5; Yn 2:24; Ufu 2:23; Amo 5:25 Tena itakuwa, wakiisha kujiliwa na mambo maovu mengi na mashaka, utashuhudia wimbo huu mbele yao kama shahidi, kwa maana hautasahauliwa katika vinywa vya uzao wao; kwani nayajua mawazo yao wayawazayo, hata sasa kabla sijawatia katika nchi niliyoapa. 22Basi Musa akauandika wimbo huu siku iyo hiyo, akawafundisha wana wa Israeli. 23#Hes 27:23; Yos 1:6 Akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia, Uwe hodari na moyo mkuu, kwa kuwa utawapeleka wana wa Israeli katika nchi niliyowaapia; nami nitakuwa pamoja nawe.
24Basi ikawa hapo Musa alipomaliza kuandika maneno ya torati hii katika kitabu, hata yakaisha, 25ndipo Musa akawaamuru Walawi waliokuwa wakilichukua sanduku la Agano la BWANA akawaambia, 26#1 Fal 8:9; 2 Fal 22:8; 2 Nya 34:14,15 Twaeni kitabu hiki cha torati, mkiweke kando ya sanduku la Agano la BWANA, Mungu wenu, ili kiwepo kama shahidi juu yako. 27#Kum 9:24; Kut 32:9; 2 Nya 30:8; Zab 78:8; Isa 48:4 Kwa kuwa uasi wako naujua, na shingo yako ngumu; angalieni, mimi ningali hai pamoja nanyi leo, mmekuwa waasi juu ya BWANA; siuze nitakapokwisha kufa! 28#Kum 30:19; 32:1 Nikutanishieni wazee wote wa makabila yenu, na maofisa wenu, ili niseme maneno haya masikioni mwao, na kuwashuhudizia mbingu na nchi juu yao. 29#Amu 2:19; Hos 9:9 Kwa sababu najua baada ya kufa kwangu mtajiharibu kabisa, na kukengeuka katika njia niliyowaamuru; nayo mabaya yatawapata siku za mwisho, kwa vile mtakavyofanya maovu machoni pa BWANA kumtia kasirani kwa kazi ya mikono yenu.
Wimbo wa Musa
30Musa akasema maneno ya wimbo huu masikioni mwa kusanyiko la wana wa Israeli hata yakaisha.
Currently Selected:
Kumbukumbu la Torati 31: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.