YouVersion Logo
Search Icon

Kumbukumbu la Torati 9

9
Matokeo ya kumuasi Mungu
1 # Kum 4:38; 7:1; 11:23; 1:28 Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo makubwa, na yenye nguvu kukupita, miji mikubwa iliyojengewa kuta hadi mbinguni, 2#Hes 13:22 watu wakubwa, warefu, wana wa Waanaki, uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, Ni nani awezaye kusimama mbele ya wana wa Anaki? 3#Kum 31:3; Yos 3:11; Mik 2:13; Ufu 19:11-15; Kum 4:24; Isa 30:27; 33:14; Nah 1:5,6; 2 The 1:8; Ebr 12:29; Kut 23:31; Kum 7:24 Basi jua siku hii ya leo kuwa BWANA, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakapowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia BWANA. 4#Kum 8:11,17; Eze 36:32; Rum 11:6; 1 Kor 4:4; Mwa 15:16; Law 18:24; Kum 18:12 Usiseme moyoni mwako, BWANA, Mungu wako, atakapokwisha kuwasukumia nje mbele yako, ukasema, Ni kwa haki yangu alivyonitia BWANA niimiliki nchi hii; kwani ni kwa ajili ya uovu wa mataifa haya BWANA anawafukuza nje mbele yako. 5#2 Tim 1:9; Tit 3:5; Mwa 12:7; 13:15; 15:7; Kut 32:13; Lk 1:54,55; Mdo 13:32,33; Rum 15:8 Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya BWANA, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno BWANA alilowaapia baba zako Abrahamu, na Isaka, na Yakobo. 6Basi jua ya kuwa BWANA, Mungu wako, hakupi nchi hii nzuri uimiliki kwa ajili ya haki yako, kwa maana u taifa lenye shingo ngumu. 7#Kut 14:11; 16:2; 17:2; Hes 11:4; 14:1; 20:2 Kumbuka, usisahau ulivyomtia BWANA, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hadi mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya BWANA 8#Kut 32:4; Zab 106:19 Tena mlimkasirisha BWANA katika Horebu, BWANA akakasirika hadi akataka kuwaangamiza. 9#Kut 24:18; 34:28; Lk 4:1 Na hapo nilipokwea mlimani kwenda kuzipokea mbao za mawe, nazo ni mbao za agano BWANA alilofanya nanyi, ndipo nikakaa mle mlimani siku arubaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji. 10BWANA akanipa vile vimbao viwili vya mawe vilivyoandikwa kwa kidole cha Mungu; na juu yake yameandikwa maneno mfano wa yote aliyosema nanyi BWANA mle mlimani kutoka kati ya moto siku ya mkutano. 11Ikawa mwisho wa siku arubaini usiku na mchana, BWANA alinipa zile mbao mbili za mawe, nazo ni mbao za agano. 12#Kut 32:7; Kum 31:29; Amu 2:17 BWANA akaniambia, Ondoka huko, shuka upesi; kwa kuwa watu wako uliowatoa Misri wamejiharibu; wamekengeuka mara katika njia niliyowaamuru; wamejifanyia sanamu ya kusubu. 13#Kut 32:9; Kum 10:16; 31:27; 2 Fal 17:14 Tena BWANA akasema nami zaidi, akaniambia, Nimeliona taifa hili; na tazama, ni taifa lenye shingo ngumu; 14#Kum 29:20; Zab 9:5; 109:13 niache, nipate kuwaangamiza, na kulifuta jina lao chini ya mbingu; nami nitakufanya wewe uwe taifa kubwa lenye nguvu kuliko wao. 15Basi nikageuka nikashuka mle mlimani, mlima ukawaka moto; na vile zile mbao mbili za agano zilikuwa katika mikono yangu miwili. 16Nikaangalia, na tazama, mlikuwa mmefanya dhambi juu ya BWANA, Mungu wenu; mmefanya ndama ya ng'ombe ya kusubu; mmepotoka punde katika njia aliyowaamuru BWANA. 17#Zab 69:9; 119:139 Nikazishika zile mbao mbili, nikazitupa kutoka katika mikono yangu miwili, nikazivunja mbele ya macho yenu. 18#Kut 34:28; Zab 106:23 Nikaanguka chini mbele za BWANA siku arubaini usiku na mchana, kama pale kwanza; sikula chakula wala kunywa maji; kwa sababu ya makosa yenu yote mliyofanya, kwa kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, kwa kumkasirisha. 19#Ebr 12:21,29; Kut 32:10,11,14; 33:17; Kum 10:10; Zab 106:23; Yak 5:15; Amo 7:1-6 Kwa kuwa niliogopa hasira na makamio aliyowakasirikia BWANA kutaka kuwaangamiza. Lakini BWANA alinisikiza wakati huo nao. 20BWANA akamkasirikia sana Haruni akataka kumwangamiza; nikamwombea Haruni naye wakati huo. 21#Kut 32:20; Isa 2:18-21; 30:22; 31:7; Hos 8:11 Kisha nikaitwaa ile dhambi yenu, huyo ndama mliyemfanya, nikamteketeza kwa moto, nikamponda, nikamsaga tikitiki, hata akawa laini kama vumbi; nikalitupa vumbi lake katika kijito kilichoshuka kutoka mlimani. 22#Hes 11:3,34; Kut 17:7 Tena huko Tabera, na Masa, na Kibroth-hataava mlimtia BWANA hasira. 23#Hes 13:3,17; 14:1; Zab 78:22; 106:24; Kum 1:21,26; Ebr 3:16; 4:2 Na wakati alipowatuma BWANA kutoka Kadesh-barnea, akiwaambia, Kweeni mkaimiliki nchi niliyowapa; ndipo mkaasi juu ya maagizo ya BWANA, Mungu wenu, hamkumsadiki wala hamkusikiza sauti yake. 24#Kum 31:27 Mmekuwa na uasi juu ya BWANA tokea siku nilipowajua ninyi. 25Ndipo nikaanguka chini mbele za BWANA siku zile arubaini usiku na mchana nilizokuwa nimeanguka chini; kwa kuwa BWANA alisema atawaangamiza. 26#Kut 32:11; 1 Sam 7:9; Mit 15:29; Yer 15:1 Nikamwomba BWANA, nikasema, Ee Bwana Mungu, usiwaangamize watu wako, urithi wako, uliowakomboa kwa ukuu wako, uliowatoa Misri kwa mkono wa nguvu. 27Wakumbuke watumishi wako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; usiangalie ukaidi wa watu hawa, wala uovu wao, wala dhambi yao; 28#Mwa 41:57; 1 Sam 14:25; Kut 32:12; Hes 14:16; Kum 32:26,27; Yos 7:7-9; Zab 115:1,2; Isa 48:9-11 isije nchi uliyotutoa ikasema, Ni kwa sababu BWANA hakuweza kuwaleta katika nchi aliyowahidi, tena ni kwa kuwa aliwachukia, aliwatoa nje ili kuwaua jangwani. 29#Kum 4:20; 1 Fal 8:51; Neh 1:10; Zab 95:7 Nao ni watu wako, urithi wako, uliowatoa kwa nguvu zako kuu na mkono wako ulionyoka.

Currently Selected:

Kumbukumbu la Torati 9: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in