YouVersion Logo
Search Icon

Kutoka 33

33
Agizo la kuondoka Sinai
1 # Mwa 12:7; 26:3; 28:13 BWANA akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii; 2#Kum 7:22; Yos 24:11 nami nitamtuma malaika aende mbele yako; nami nitawafukuza Mkanaani, na Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi; 3#Kut 32:9; Kum 9:6 waifikie nchi imiminikayo maziwa na asali; kwa maana mimi sitakwenda kati yenu; kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu; nisiwaangamize ninyi katika njia. 4#2 Sam 19:24 Watu waliposikia habari hizo mbaya wakaomboleza wala hakuna mtu aliyevaa mapambo yake. 5#Kut 32:9; Zab 139:23 BWANA akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli, Ninyi ni watu wenye shingo ngumu; kama mimi nikiingia kati yenu dakika moja, nitawaangamiza; basi sasa vueni mapambo yenu ili nipate kujua nitakalowatenda. 6Basi wana wa Israeli wakavua mapambo yao, tangu mlima wa Horebu na mbele.
Hema nje ya kambi
7 # 2 Sam 21:1 Basi desturi ya Musa, ilikuwa kuitwaa ile hema, na kuikita nje ya kambi na mbali hiyo kambi; akaiita, hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa BWANA, akatoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya kambi. 8#Hes 16:27 Hata Musa alipotoka kuiendea ile hema, watu wote waliondoka wakasimama, kila mtu mlangoni pa hema yake, akamtazama Musa, hata alipokwisha kuingia hemani. 9#Zab 99:7 Ikawa Musa alipoingia humo hemani, ile nguzo ya wingu ikashuka, ikasimama mlangoni pa ile hema; naye BWANA akasema na Musa. 10Watu wote wakaiona nguzo ya wingu ikisimama penye mlango wa hema; watu wote wakaondoka wakasujudu, kila mtu mlangoni pa hema yake. 11#Mwa 32:30; Kum 5:24; 34:10; Kut 24:13 Naye BWANA akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata kambini; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani.
Maombezi ya Musa kwa Mungu
12 # Zab 1:6; Yer 1:5; Yn 10:14; 2 Tim 2:19 Musa akamwambia BWANA, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Lakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu. 13#Kut 34:9; Zab 25:4; 27:11; Kum 9:26; Yoe 2:17 Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unioneshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. 14#Kut 40:34-38; Isa 63:9; Kum 3:20; Yos 21:44; 22:4; 23:1; Zab 95:11 Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. 15#Kut 34:9 Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. 16#Hes 14:14; Kum 4:34; 2 Sam 7:23; Zab 147:20; Tit 2:14 Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi? 17#Mwa 19:21; Yak 5:16 BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako. 18#1 Tim 6:16 Akasema, Nakusihi unioneshe utukufu wako. 19#Rum 9:1,15; 4:4; Yer 31:14 Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu. 20#Mwa 32:30; Kum 5:24; Amu 13:22; Isa 6:5; Ufu 1:16 Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi. 21BWANA akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba; 22#Isa 2:21; Zab 91:1,4 kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita; 23#Yn 1:18; 1 Tim 6:16; 1 Yoh 1:2 nami nitaondoa mkono wangu, nawe utaniona nyuma yangu, bali uso wangu hautaonekana.

Currently Selected:

Kutoka 33: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in