Ezekieli 29
29
Utabiri juu ya Misri
1 #
Isa 19:1-25; Yer 46:2-26 Katika mwaka wa kumi, mwezi wa kumi, siku ya kumi na mbili ya mwezi, neno la BWANA likanijia, kusema, 2#Isa 19:1; Yer 25:19 Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Farao, mfalme wa Misri, ukatabiri juu yake, na juu ya Misri yote; 3#Yer 44:30; Zab 74:13,14; Eze 28:2,22; 32:2; Isa 27:1 nena, useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Farao, mfalme wa Misri, joka kubwa aoteaye kati ya mito yake, aliyesema, Mto wangu ni wangu mwenyewe, nami nimeufanya kwa ajili ya nafsi yangu. 4#2 Fal 19:28; Isa 37:29; Eze 38:4 Nami nitatia kulabu katika taya zako, nami nitawashikamanisha samaki wa mito yako na magamba yako; nami nitakutoa katika mito yako, pamoja na samaki wa mito yako walioshikamana na magamba yako. 5#Yer 8:2; 7:33 Nami nitakuacha ukiwa umetupwa jangwani, wewe na samaki wote wa mito yako; utaanguka katika uwanda ulio wazi; hutakusanywa, wala kuwekwa pamoja; nimekutoa uwe chakula cha wanyama wa nchi, na cha ndege wa angani. 6#2 Fal 18:21; Isa 36:6 Na watu wote wakaao Misri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, kwa sababu wamekuwa mwanzi wa kutegemewa kwa nyumba ya Israeli. 7#Yer 37:5 Walipokushika kwa mkono wako, ulivunjika, ukawararua mabega yao yote; nao walipokutegemea, ulivunjika, ukawatetemesha viuno vyao vyote. 8Basi, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitaleta upanga juu yako, nami nitakatilia mbali nawe wanadamu na wanyama. 9#Mit 16:18 Nayo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA; kwa sababu amesema, Mto huu ni wangu, nami nimeufanya. 10#Eze 30:12 Basi, tazama, mimi ni juu yako, na juu ya mito yako, nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa jangwa tupu, na ukiwa, toka Migdoli hata Sewene, hata mpaka wa Kushi. 11#Yer 43:11,12; Eze 30:10-13 Hautapita kati yake mguu wa mwanadamu, wala hautapita kati yake mguu wa mnyama, wala haitakaliwa na watu, muda wa miaka arubaini. 12#Yer 25:17,18; Eze 30:7 Nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa, kati ya nchi zilizo ukiwa, na miji yake, kati ya miji iliyoharibika, itakuwa maganjo muda wa miaka arubaini; nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa, nami nitawatapanya kati ya nchi mbalimbali. 13#Isa 19:23; Yer 46:25,26 Maana Bwana MUNGU asema hivi; Mwisho wa miaka arubaini nitawakusanya Wamisri, na kuwatoa katika hayo makabila ya watu, ambazo walitawanyika kati yao; 14nami nitawarejesha Wamisri walio katika hali ya kufungwa, nami nitawarudisha Pathrosi, nchi ya kuzaliwa kwao; na huko watakuwa ufalme duni. 15Utakuwa duni kuliko falme zote; wala hautajiinua tena juu ya mataifa; nami nitawapunguza, ili wasitawale tena juu ya mataifa. 16#Isa 30:2; Yer 2:18,19; Omb 4:17 Wala hautakuwa tena tegemeo la nyumba ya Israeli, kufanya maovu yakumbukwe, watakapogeuka kuangalia nyuma yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.
Babeli waiteka Misri
17Ikawa katika mwaka wa ishirini na saba, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, neno la BWANA likanijia, kusema, 18#Yer 27:6; Eze 26:7 Mwanadamu, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alilifanyisha jeshi lake kazi ngumu juu ya Tiro; kila kichwa kilitiwa upara, na kila bega liliambuliwa ngozi, lakini hakuna mshahara uliotoka Tiro, sio wake wala wa jeshi lake, kwa kazi ile aliyofanya juu yake. 19Basi, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitampa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, hiyo nchi ya Misri; naye atawachukua watu wake jamii yote pia, na kutwaa mateka yake, na kutwaa mawindo yake, nayo yatakuwa ndio mshahara wa jeshi lake. 20#Yer 25:9 Nimempa nchi ya Misri kuwa malipo ya kazi aliyofanya, kwa sababu walifanya kazi kwa ajili yangu; asema Bwana MUNGU.
21 #
1 Sam 2:10; Zab 132:17; Mwa 18:17; Eze 3:26; Amo 3:7; Dan 9:22-27 Siku ile nitawachipushia nyumba ya Israeli pembe, nami nitakujalia kufumbua kinywa kati yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.
Currently Selected:
Ezekieli 29: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.