YouVersion Logo
Search Icon

Wagalatia 5

5
1 # Gal 4:5,31; Mdo 15:10 Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.
Asili ya uhuru wa Mkristo
2 # 2 Kor 10:1 Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidi neno. 3Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote. 4Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. 5Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. 6#Gal 6:15; 1 Kor 7:19 Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutotahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
7Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli? 8#Gal 1:6 Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi. 9#1 Kor 5:6 Chachu kidogo huchachua donge zima. 10#Gal 1:7; 2 Kor 11:15 Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewasumbua atachukua hukumu yake, awaye yote. 11#1 Kor 1:23 Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Kwa kufanya hivyo kikwazo cha msalaba kimeondolewa! 12#Zab 12:3 Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao!
13 # 1 Pet 2:16 Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. 14#Law 19:18 Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako. 15Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.
Kazi za kimwili
16Basi nasema, Nendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17#Rum 7:15-23; Yak 4:5; 1 Pet 2:11 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18#Rum 8:14 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. 19#1 Kor 6:9,10 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, 21#Efe 5:5; Ufu 22:15 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tunda la Roho
22 # Efe 5:9 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23#1 Tim 1:9 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. 24#Rum 6:6; Kol 3:5; 1 Pet 2:11 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. 25#Rum 8:4 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. 26#Flp 2:3 Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.

Currently Selected:

Wagalatia 5: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Wagalatia 5