YouVersion Logo
Search Icon

Mwanzo 29

29
Yakobo akutana na Raheli
1 # Hes 23:7; Hos 12:12 Kisha Yakobo akashika njia yake, akafika nchi ya wana wa mashariki.
2Naye akaangalia, na tazama, kiko kisima kondeni, na makundi matatu ya kondoo yamelala karibu nacho, kwa sababu katika kisima kile hunywesha makundi; na palikuwa na jiwe kubwa juu ya kinywa cha kisima. 3Makundi yote hukusanyika huko, watu wakabingirisha hilo jiwe katika kinywa cha kisima wakawanywesha kondoo, na kulirudisha jiwe juu ya kinywa cha kisima mahali pake. 4Yakobo akawauliza, Ndugu zangu, ninyi ni watu wa wapi? Wakasema, Sisi tu wa Harani. 5Akawauliza, Je! Mnamjua Labani, mwana wa Nahori? Wakasema, Tunamjua. 6#Mwa 43:27 Akawauliza, Je! Hajambo? Wakasema, Hajambo; tazama, Raheli binti yake anakuja na kondoo. 7Akasema, Tazama, kungali mchana bado, wala sio wakati wa kukusanya wanyama; wanywesheni kondoo, mwende kuwalisha. 8Wakasema, Hatuwezi, Mpaka makundi yote yakusanyike, watu wakabingirishe jiwe katika kinywa cha kisima, ndipo tunapowanywesha kondoo.
9 # Kut 2:16 Na alipokuwa akisema nao, Raheli akaja na kondoo wa baba yake, maana aliwachunga. 10#Kut 2:17 Ikawa Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mamaye, na kondoo wa Labani, ndugu wa mamaye, Yakobo akakaribia, na kulibingirisha lile jiwe litoke katika kinywa cha kisima, akawanywesha kondoo wa Labani, ndugu wa mamaye.
11 # Mwa 33:4; 45:14; Rum 16:16; 1 Kor 16:20; 2 Kor 13:12; 1 Pet 5:14 Yakobo akambusu Raheli, akalia kwa sauti. 12#Mwa 13:8; 24:28 Yakobo akamwarifu Raheli ya kuwa yeye ni ndugu wa babaye, na ya kuwa ni mwana wa Rebeka. Basi akapiga mbio akampasha babaye habari. 13#Mwa 24:29 Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote. 14#Mwa 2:23; Amu 9:2; 2 Sam 5:1; 19:12,13 Labani akamwambia, Ndiwe kweli mfupa wangu na nyama yangu. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja.
Yakobo awaoa mabinti wa Labani
15Labani akamwambia Yakobo, Kwa sababu wewe ni jamaa yangu, basi, je! Unitumikie bure? Niambie mshahara wako utakuwa nini? 16Labani alikuwa na binti wawili, jina la mkubwa ni Lea, na jina la mdogo ni Raheli. 17Naye Lea macho yake yalikuwa malegevu,#29:17 Maana katika Kiebrania si dhahiri. lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri wa uso. 18#Mwa 31:41; 2 Sam 3:14 Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo. 19Labani akasema, Afadhali nikupe wewe kuliko mtu mwingine; kaa kwangu. 20#Mwa 30:26; Wim 8:7 Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda. 21#Amu 15:1 Yakobo akamwambia Labani, Nipe mke wangu, maana siku zangu zimetimia; niingie kwake. 22#Amu 14:10; Yn 2:1 Labani akakusanya watu wote wa mahali pale, akafanya karamu. 23Ikawa wakati wa jioni akamtwaa Lea, binti yake, akamletea Yakobo, naye akaingia kwake. 24Labani akampa Lea mjakazi wake Zilpa, awe mjakazi wake. 25Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda? 26Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa; 27#Amu 14:12 timiza siku zake saba, nasi tutakupa huyu naye kwa utumishi utakaonitumikia, miaka saba mingine.
28Yakobo akafanya hivi, akatimiza siku zake saba. Naye Labani#29:28 Katika Kiebrania hakuna Labani. akampa Raheli, binti yake, kuwa mkewe. 29Labani akampa binti yake Raheli mjakazi wake Bilha, awe mjakazi wake. 30#Mwa 30:26; 31:41; Hos 12:12 Ndipo Yakobo#29:30 Katika Kiebrania hakuna Yakobo. akaingia kwa Raheli, akampenda Raheli kuliko Lea, akatumika kwa ajili yake miaka saba mingine.
31 # Zab 127:3; Mwa 30:1 BWANA akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai. 32#Kut 3:7; 4:31; Kum 26:7; Zab 25:18; 106:44 Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa BWANA ameona mateso yangu; sasa mume wangu atanipenda. 33Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa BWANA amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni. 34Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi. 35Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu BWANA; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa.

Currently Selected:

Mwanzo 29: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in