Mwanzo 33
33
Yakobo na Esau wakutana
1 #
Mwa 32:6
Yakobo akainua macho yake, akaona, na tazama, Esau anakuja na watu mia nne pamoja naye. Akawagawanyia Lea, na Raheli, na wale vijakazi wawili, wana wao. 2Akawaweka hao vijakazi na wana wao mbele, na Lea na wanawe nyuma yao, na Raheli na Yusufu mwisho. 3#Mwa 18:2; 42:6 Akapita mwenyewe mbele yao, akainama mpaka nchi mara saba, hata alipomkaribia ndugu yake. 4#Mwa 32:28; Mit 16:1; 21:1; Yer 10:23 Esau akaja mbio kumlaki, akamkumbatia, na kumwangukia shingoni, akambusu; nao wakalia. 5#Mwa 48:9; Zab 127:3; Isa 8:18 Akainua macho yake, akawaona wale wanawake na watoto, akauliza, Ni nani hawa walio pamoja nawe? Akasema, Ni watoto Mungu aliompa mtumwa wako kwa neema yake. 6Ndipo wale vijakazi, na wana wao, wakakaribia wakainama. 7Lea naye, na wanawe, wakakaribia wakainama. Baadaye Yusufu na Raheli wakakaribia, wakainama.
8 #
Mwa 32:5,16 Akasema, Kundi hili lote nililokutana nalo, maana yake ni nini? Akasema, Ili kunipatia kibali machoni pa bwana wangu. 9Esau akasema, Ninayo tele, ndugu yangu, hifadhi uliyo nayo yawe yako. 10#Mwa 43:3; 2 Sam 3:13; 14:24-32; Mt 18:10 Yakobo akasema, Sivyo; nakuomba kama nimekubalika machoni pako tafadhali upokee zawadi yangu mkononi mwangu, Hakika, kuona uso wako ni kama kuuona uso wa Mungu – maana umenipokea kwa kibali kama chake. 11#Amu 1:15; 1 Sam 25:27; 2 Fal 5:15; Flp 4:18; 2 Fal 5:23 Tafadhali pokea zawadi yangu iliyoletwa kwako, kwa sababu Mungu amenineemesha, na kwa sababu ninavyo hivi vyote. Akamsihi sana, naye akapokea.
12Kisha Esau akamwambia, Twende zetu, tusafiri, nami nitakutangulia. 13Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto ni wachanga, tena kondoo na ng'ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama wakiharakishwa siku moja, watakufa wote. 14#Mwa 32:3 Tafadhali bwana wangu na apite mbele ya mtumwa wake; nami nitawaongoza polepole kwa kadiri ya mwendo wa wanyama walio mbele yangu, na kwa kadiri ya mwendo wa watoto, hadi nitakapofika kwa bwana wangu huko Seiri. 15#Rut 2:13 Esau akasema, Basi nikuachie, baadhi ya watu walio pamoja nami. Akasema, Pana haja gani? Na nione kibali tu machoni pa bwana wangu. 16Basi Esau akarudi siku ile ile akishika njia yake mpaka Seiri. 17#Yos 13:27; Amu 8:5 Yakobo akaendelea mpaka Sukothi. Akajijengea nyumba, akawafanyia makundi yake vibanda. Kwa hiyo jina la mahali pale pakaitwa Sukothi.
Yakobo afika Shekemu
18 #
Yn 3:23; Mdo 7:16; Yos 24:1 Yakobo akaja kwa amani mpaka katika mji wa Shekemu, ulio katika nchi ya Kanaani, alipokuja kutoka Padan-aramu; akapiga kambi mbele ya huo mji. 19#Yos 24:32; Yn 4:5; Mdo 7:16 Akainunua sehemu ya nchi, alipopiga hema yake, kwa mkono wa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa vipande mia moja vya fedha. 20#Mwa 35:7 Akajenga huko madhabahu, akaiita, El-elohe-Israeli.#33:20 El-elohe-Israeli: maana yake ni Mungu, Mungu wa Israeli.
Currently Selected:
Mwanzo 33: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.