YouVersion Logo
Search Icon

Mwanzo 46

46
Yakobo ahamia Misri na jamaa yake yote
1 # Mwa 21:31; 26:24; 28:13; 31:42 Israeli Akasafiri, pamoja na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka babaye. 2#Mwa 15:1; Ayu 33:14,15 Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa. 3#Mwa 12:2; 28:13; Kum 26:5; Kut 1:9 Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko. 4#Mwa 28:15; 48:21; 15:16; 50:13; Kut 3:8 Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako. 5#Mwa 15:13; Mdo 7:15 Yakobo akaondoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyotuma Farao ili kumchukua. 6#Kum 26:5; Yos 24:4; Zab 105:23; Isa 52:4 Wakatwaa na wanyama wao, na mali zao walizokuwa wamepata katika nchi ya Kanaani, wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye. 7Wanawe, na wana wa wanawe, pamoja naye, binti zake na binti za wanawe, na uzao wake wote, aliwaleta pamoja naye mpaka Misri.
8 # Kut 1:1; 6:14; Hes 26:5; 1 Nya 5:1 Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli walioingia Misri, Yakobo na wanawe: Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. 9Na wana wa Reubeni; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi. 10#Kut 6:15; 1 Nya 4:24 Na wana wa Simeoni; Yemueli na Yamini, na Ohadi, na Yakini, na Sohari, na Shauli, mwana wa mwanamke Mkanaani. 11Na wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari. 12#Mwa 38:3,29; 1 Nya 2:5 Na wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela, na Peresi, na Zera; lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Peresi, ni Hesroni, na Hamuli. 13Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni. 14Na wana wa Zabuloni; Seredi, na Eloni, na Yaleeli. 15Hao ndio wana wa Lea, aliomzalia Yakobo katika Padan-aramu, na Dina, binti yake. Wanawe wote wa kiume na kike walikuwa watu thelathini na watatu. 16#Hes 26:15 Na wana wa Gadi; Sefoni, na Hagi, na Shuni, na Esboni, na Eri, na Arodi, na Areli. 17#1 Nya 7:30 Na wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na Sera, dada yao. Na wana wa Beria ni Heberi, na Malkieli. 18#Mwa 30:10 Hao ndio wana wa Zilpa, ambaye Labani alimpa Lea, binti yake, naye akamzalia Yakobo hao, watu kumi na sita. 19Wana wa Raheli, mkewe Yakobo, Yusufu na Benyamini. 20#Mwa 41:50-52 Walizaliwa kwake Yusufu katika nchi ya Misri, Manase na Efraimu, aliomzalia Asenathi binti Potifera, kuhani wa Oni. 21#1 Nya 7:6,12 Na wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Ashbeli, na Gera, na Naamani, na Ehi, na Roshi, na Mupimu, na Hupimu, na Ardi. 22Hao ndio wana wa Raheli, aliomzalia Yakobo, wote walikuwa watu kumi na wanne. 23#1 Nya 7:12 Na wana wa Dani; Hushimu. 24#1 Nya 7:13 Na wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yaseri, na Shilemu. 25#Mwa 29:29; 30:5,7 Hao ndio wana wa Bilha, ambaye Labani alimpa Raheli, binti yake, naye akamzalia Yakobo hao; wote walikuwa watu saba.
26 # Kut 1:5 Watu wote waliokuja pamoja na Yakobo mpaka Misri, waliokuwa wazawa wake, bila wake za wanawe, walikuwa watu sitini na sita. 27#Mdo 7:14; Kum 10:22 Na wana wa Yusufu aliozaliwa katika Misri walikuwa wawili. Watu wote wa nyumba ya Yakobo walioingia Misri walikuwa sabini.
Yakobo apata makao Gosheni
28 # Mwa 31:21 Yakobo akamtuma Yuda mbele yake kwa Yusufu, ili amwongoze njia mpaka Gosheni. Wakaja mpaka nchi ya Gosheni. 29Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kirefu. 30#Lk 2:29 Israeli akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya kuwa ungali hai. 31Yusufu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, Nitapanda mimi nimpashe Farao habari; nitamwambia, Ndugu zangu, na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa katika nchi ya Kanaani, wamenijia. 32Na watu hao ni wachungaji, maana wamekuwa watu wa kuchunga wanyama, nao wameleta kondoo zao, na ng'ombe zao, na yote waliyo nayo. 33#Mwa 47:2,3 Itakuwa Farao atakapowaita, na kuwauliza, Kazi yenu ni nini? 34#Mwa 30:35; 34:5; 37:12; Kut 8:26 Semeni, Watumishi wako tumekuwa wachunga wanyama tangu ujana wetu, na hata leo, sisi, na baba zetu; mpate kukaa katika nchi ya Gosheni; maana kila mchunga wanyama ni chukizo kwa Wamisri.

Currently Selected:

Mwanzo 46: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in