YouVersion Logo
Search Icon

Hosea 8

8
Uasi wa Israeli
1 # Yer 4:13; Hab 1:8 Tia baragumu kinywani mwako. Kama tai, anakuja juu ya nyumba ya BWANA; kwa sababu wamelivunja agano langu, wameiasi sheria yangu. 2#Zab 78:34; Mt 7:21 Watanililia, Mungu wangu, sisi Israeli tunakujua. 3Israeli ameyatupa yaliyo mema; adui watamfuatia. 4#1 Fal 12:16-20; 2 Fal 15:13,17,25 Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nilikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali. 5#Yer 13:27 Ndama wako amemtupa, Ee Samaria; ghadhabu yangu imewaka juu yao; Wataendelea kuwa na hatia hadi lini? 6Maana katika Israeli kimetokea hata na kitu hiki; fundi ndiye aliyekifanya, nacho si mungu kamwe; naam, ndama ya Samaria itavunjika vipande vipande.
7Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza. 8Israeli amemezwa; sasa wamo miongoni mwa mataifa kama chombo kisichopendeza. 9#2 Fal 15:19 Kwa maana wamekwea kwenda Ashuru, mfano wa punda wa porini aliye peke yake; Efraimu ameajiri wapenzi. 10#Isa 10:8; Eze 26:7; Dan 2:37 Naam, ijapokuwa waajiri kati ya mataifa, sasa nitawakusanya; nao wanaanza kupunguka kwa sababu ya mzigo wa mfalme wa wakuu. 11Kwa kuwa Efraimu ameongeza madhabahu kwa dhambi, madhabahu zimekuwa dhambi kwake. 12#Kum 4:6; Neh 9:13,14; Mit 22:20; Rum 3:1,2; Ayu 21:14 Nijapomwandikia sheria yangu katika amri makumi elfu, zimehesabiwa kuwa ni kitu kigeni. 13Kwa habari za dhabihu za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini BWANA hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao; watarudi kwenda Misri. 14#1 Fal 12:31 Maana Israeli amemsahau Muumba wake, naye amejenga nyumba za enzi; na Yuda ameongeza miji yenye maboma; lakini nitatuma moto juu ya miji yake, nao utaziteketeza ngome zake.

Currently Selected:

Hosea 8: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Hosea 8