YouVersion Logo
Search Icon

Isaya 31

31
Kuungana na Misri ni bure
1 # Kum 28:68; Eze 17:15; Hos 11:8; Zab 20:7; Dan 9:13; Hos 7:7 Ole wao wateremkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti BWANA! 2Lakini yeye naye ana akili, naye ataleta uovu, wala hatayatangua maneno yake; bali ataondoka juu ya nyumba yao watendao mabaya, na juu ya msaada wa hao watendao maovu. 3#Zab 9:20; Eze 28:9 Basi Wamisri ni wanadamu wala si Mungu, na farasi wao ni nyama wala si roho; na BWANA atakaponyosha mkono wake, yeye asaidiaye atajikwaa, na yeye asaidiwaye ataanguka, nao wataangamia wote pamoja. 4Maana BWANA aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwanasimba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo BWANA wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake. 5#Kum 32:11; Zab 91:4 Kama ndege warukao, BWANA wa majeshi ataulinda Yerusalemu; ataulinda na kuuokoa, atapita juu yake na kuuhifadhi. 6#Hos 9:9 Mwelekeeni yeye mliyemwasi sana, enyi wana wa Israeli. 7#1 Fal 12:30 Maana katika siku hiyo kila mtu atatupa sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, ambazo mikono yenu imezifanya, zikawa dhambi kwenu. 8#2 Fal 19:35 Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamwangamiza; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi. 9#Law 6:13 Na mwamba wake utatoweka kwa sababu ya hofu, nao wakuu wake wataionea bendera hofu kuu, asema BWANA, ambaye moto wake u katika Sayuni, na tanuri yake katika Yerusalemu.

Currently Selected:

Isaya 31: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in