YouVersion Logo
Search Icon

Yeremia 22

22
Mahimizo ya toba
1BWANA akasema hivi, Shuka nyumbani kwa mfalme wa Yuda, ukaseme neno hili huko, 2ya kwamba, Sikia neno la BWANA, Ee mfalme wa Yuda; wewe uketiye katika kiti cha enzi cha Daudi, wewe, na watumishi wako, na watu wako wote waingiao kwa malango haya; 3#Isa 58:6,7; Yer 7:23; Mik 6:8; Zek 7:9; Mt 23:23 BWANA asema hivi, Fanyeni hukumu na haki, mkamtoe yeye aliyetekwa katika mikono ya mdhalimu; wala msiwatende mabaya mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kuwadhulumu, wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia katika mahali hapa. 4#Yer 17:25 Kwa maana mkifanya haya kweli kweli, ndipo watakapoingia kwa malango ya nyumba hii wafalme wenye kuketi katika kiti cha enzi cha Daudi, wanakwenda kwa magari, na wamepanda farasi, yeye, na watumishi wake, na watu wake. 5#Hes 23:19; 1 Sam 15:29; Zab 95:11; Amo 6:8; Ebr 3:18; Mt 23:38; Lk 13:35 Lakini kama hamtaki kusikia maneno haya, mimi naapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, ya kuwa nyumba hii itakuwa ukiwa. 6#Mik 3:12 Kwa maana BWANA asema hivi, kuhusu habari za nyumba ya mfalme wa Yuda;
Wewe u Gileadi kwangu,
na kichwa cha Lebanoni;
Ila hakika nitakufanya kuwa jangwa,
na miji isiyokaliwa na watu.
7 # Isa 37:24; Yer 21:14 Nami nitawatayarisha waangamizi juu yako,
kila mtu na silaha zake;
Nao watakata mierezi yako miteule,
na kuitupa motoni.
8 # Kum 29:24; 1 Fal 9:8 Na mataifa mengi watapita karibu na mji huu, nao watasema kila mtu na jirani yake, Nini maana yake BWANA kuutenda hivi mji huu mkubwa? 9#2 Fal 22:17; 2 Nya 34:25 Ndipo watakapojibu, Ni kwa sababu waliliacha agano la BWANA, Mungu wao, wakaabudu miungu mingine, na kuitumikia.
10 # 2 Fal 22:20; Isa 57:1,21 Msimlilie aliyekufa, wala msimwombolezee,
Bali mlilieni huyo aendaye zake mbali;
Kwa maana yeye hatarudi tena,
Wala hataiona nchi aliyozaliwa.
Ujumbe kwa wana wa Yoashi
11 # 1 Nya 3:15; 2 Fal 23:31-34; 2 Nya 36:1-4 Maana BWANA asema hivi, kuhusu habari za Shalumu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; aliyemiliki badala ya Yosia, baba yake, yeye aliyetoka mahali hapa; Hatarudi huku tena; 12bali katika mahali pale walipomchukua mateka ndipo atakapokufa, wala hataiona nchi hii tena kamwe.
13 # Law 19:13; Mik 3:10; Hab 2:9; Yak 5:4 Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu!
Na vyumba vyake kwa udhalimu!
Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira,
Wala hampi mshahara wake;
14Asemaye, Nitajijengea nyumba kubwa yenye vyumba vipana;
Naye hujikatia madirisha;
Na kuta zake zimefunikwa kwa mierezi,
Na kupakwa rangi nyekundu.
15 # Zab 128:2; Isa 3:10 Je! Utatawala kwa sababu unashindana na watu kwa mierezi? Baba yako, je! Hakula na kunywa, na kufanya hukumu na haki? Hapo ndipo alipofanikiwa. 16#1 Nya 28:9; Zab 9:10; Yn 8:19; Tit 1:16; Yak 1:22; 1 Yoh 2:3 Alihukumu maneno ya maskini na mhitaji; hapo ndipo alipofanikiwa. Je! Huku siko kunijua, asema BWANA? 17#Eze 19:6 Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia, na kudhulumu, na kutenda jeuri. 18#1 Fal 13:30; 2 Fal 23:36—24:6; 2 Nya 36:5-7 Basi, BWANA asema hivi, kuhusu habari za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake. 19#2 Nya 36:6 Atazikwa maziko ya punda, akibururwa, na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.
20Haya panda Lebanoni, ukalie
Upalize sauti yako katika Bashani;
Ukalie kutoka Abarimu;
Maana wapenzi wako wote wameangamia.
21 # Yer 3:25 Mimi nilisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutoitii sauti yangu. 22#Yer 23:1 Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na wapenzi wako watakwenda kufungwa; hakika wakati huo utatahayarika, na kufadhaika kwa sababu ya uovu wako wote.
23 # Yer 6:24 Wewe ukaaye Lebanoni,
Ujengaye kiota chako katika mierezi,
Utakuwa na hali ya kuhurumiwa sana,
Upatapo uchungu kama wa mwanamke azaaye.
Hukumu kwa Konia
24 # 2 Fal 24:6,8-15; 1 Nya 3:16; Wim 8:6; Hag 2:23; 2 Nya 36:9-10 Kama niishivyo mimi, asema BWANA, hata Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, angekuwa pete yenye mhuri katika mkono wangu wa kulia, ningekung'oa wewe hapo; 25#Yer 34:20 nami nitakutia katika mikono ya watu wale wakutafutao roho yako, na katika mikono yao unaowaogopa, naam, katika mikono ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya Wakaldayo. 26#2 Fal 24:15 Nami nitakutupa nje, wewe na mama yako aliyekuzaa, mwende katika nchi nyingine ambayo hamkuzaliwa huko, nanyi mtakufa huko. 27Lakini nchi ile ambayo wanatamani kuirudia, hawatairudia kamwe. 28#Zab 31:12; Yer 48:38 Je! Mtu huyu, Konia, ni chombo kilichodharauliwa, na kuvunjika? Ni chombo kisichopendeza? Mbona wametupwa, yeye na wazao wake, na kutupwa katika nchi wasiyoijua? 29Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la BWANA. 30BWANA asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.

Currently Selected:

Yeremia 22: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Yeremia 22