YouVersion Logo
Search Icon

Yeremia 27

27
Ishara ya nira
1 # Yer 28:1; 2 Fal 24:18-20; 2 Nya 36:11-13 Mwanzo wa kumiliki kwake Sedekia, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hili likamjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, kusema, 2#Yer 28:10; Eze 4:1 BWANA ameniambia hivi, Jitengenezee vifungo na nira, ukajivike shingoni; 3kisha uvipeleke kwa mfalme wa Edomu, na mfalme wa Moabu, na mfalme wa wana wa Amoni, na mfalme wa Tiro, na mfalme wa Sidoni, kwa mikono ya wajumbe watakaofika Yerusalemu kwa Sedekia, mfalme wa Yuda. 4Uwaagize waende kwa bwana zao, na kuwaambia, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Mtawaambia bwana zenu maneno haya; 5#Zab 96:5; 115:15,16; Isa 42:5; 45:12; Mwa 1:29,30; Kum 2:5; Yos 1:2,3; Dan 4:17 Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio katika nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo. 6#Yer 28:14; Dan 2:37,38; Yer 25:9; 43:10; Zab 50:10-12 Na sasa nimetia nchi hizi zote katika mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu; na wanyama pori pia nimempa wamtumikie. 7#2 Nya 36:20; Dan 5:26; Yer 25:12; 50:27 Na mataifa yote watamtumikia yeye, na mwanawe, na mwana wa mwanawe, hata utakapowadia wakati wa nchi yake mwenyewe, ndipo mataifa mengi na wafalme wakuu watamtumikisha yeye. 8Na itakuwa, taifa lile na mfalme yule asiyetaka kumtumikia Nebukadneza, huyo mfalme wa Babeli, na kutia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, mimi nitaliadhibu taifa lile kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, asema BWANA, hata nitakapokuwa nimewaangamiza kwa mkono wake. 9#Mit 19:27; Yer 14:14; Mik 3:7; Efe 5:6 Lakini, kuhusu habari zenu, msisikilize manabii wenu, wala wabashiri wenu, wala ndoto zenu, wala watambuzi wenu, wala waganga wenu, wanaowaambia, ya kwamba, Hamtamtumikia mfalme wa Babeli; 10maana wanawatabiria uongo, ili kuwatoa ninyi mbali na nchi yenu; niwafukuze mkaangamie. 11Bali taifa lile watakaotia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, na kumtumikia, taifa hilo nitawaacha wakae katika nchi yao wenyewe, asema BWANA; nao watailima, na kukaa ndani yake.
12 # Yer 28:1; 38:17 Nikamwambia Sedekia, mfalme wa Yuda, kwa mfano wa maneno hayo yote, nikisema, Tieni shingo zenu katika nira ya mfalme wa Babeli, mkamtumikie yeye na watu wake, mpate kuishi. 13#Mit 8:36; Eze 18:31 Mbona mnataka kufa, wewe na watu wako, kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, kama BWANA alivyosema katika habari ya taifa lile, lisilotaka kumtumikia mfalme wa Babeli? 14#Yer 14:14; 23:21 Wala msisikilize maneno ya manabii wawaambiao ninyi, ya kwamba, Hamtamtumikia mfalme wa Babeli; maana wanawatabiria uongo. 15Kwa maana mimi sikuwatuma, asema BWANA, bali wanatabiri uongo kwa jina langu; nipate kuwatoeni nje, mkaangamie, ninyi, na manabii hao wanaowatabiria. 16#2 Fal 24:13; Yer 28:3; Dan 1:2 Pia nilisema na makuhani, na watu wote, nikisema, BWANA asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wenu, wanaowatabiria, wakisema, Tazameni, vyombo vya nyumba ya BWANA, baada ya muda kidogo, vitaletwa tena toka Babeli; maana wanawatabiria uongo. 17#Eze 18:31 Msiwasikilize; mtumikieni mfalme wa Babeli, mkaishi; kwa nini mji huu ufanywe kuwa ukiwa? 18#Mwa 20:7; Ayu 42:8; Isa 37:4; Yak 5:16 Lakini ikiwa hao ni manabii, na ikiwa neno la BWANA liko kwao, basi na wamwombe BWANA wa majeshi, kwamba vyombo vile vilivyosalia katika nyumba ya BWANA, na katika nyumba ya mfalme wa Yuda, na hapa Yerusalemu, visiende Babeli. 19#2 Fal 25:13; Yer 52:17 Maana BWANA wa majeshi asema hivi, kuhusu habari za nguzo, na kuhusu habari za bahari, na kuhusu habari za vilingo vyake, na kuhusu habari za mabaki ya vyombo vilivyoachwa katika mji huu, 20#2 Fal 24:14,15; Yer 24:1 ambavyo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, hakuvichukua, hapo alipomchukua Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, toka Yerusalemu mpaka Babeli, pamoja na wakuu wote wa Yuda, na Yerusalemu; 21#Law 26:24; Isa 5:25 naam, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, katika habari za vyombo vilivyobaki katika nyumba ya BWANA, na katika nyumba ya mfalme wa Yuda, na hapa Yerusalemu; 22#2 Nya 36:21; Dan 9:2; Yer 29:10; 32:5; Ezr 1:7 Vitachukuliwa mpaka Babeli, navyo vitakaa huko, hata siku ile nitakapovijia, asema BWANA; hapo ndipo nitakapovileta tena, na kuvirudisha mahali hapa.

Currently Selected:

Yeremia 27: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Yeremia 27