YouVersion Logo
Search Icon

Yeremia 40

40
Yeremia wakiwa na mtawala Gedalia
1 # Yer 39:14 Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, baada ya wakati ule Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, alipomwacha aende zake toka Rama, baada ya kumchukua akiwa amefungwa minyororo, pamoja na wafungwa wote wa Yerusalemu na Yuda, waliochukuliwa wakiwa wamefungwa mpaka Babeli. 2#Law 26:14-38; Kum 28:15-68; 32:19-25; Yer 50:7; Omb 2:17 Naye mkuu wa askari walinzi akamtwaa Yeremia, akamwambia, BWANA, Mungu wako, alitamka mabaya haya juu ya mahali hapa; 3#Kum 29:24,25 naye BWANA ameyaleta, na kufanya kama alivyosema; kwa sababu mmemwasi BWANA, wala hamkuitii sauti yake; ndiyo maana neno hili limewajia ninyi. 4#Yer 39:12; Mwa 13:9; 20:15 Na sasa, tazama, nakufungulia leo minyororo hii iliyo mikononi mwako. Kama ukiona ni vema kwenda Babeli pamoja nami, haya! Njoo, nami nitakutunza sana; lakini kama ukiona ni vibaya kwenda Babeli pamoja nami, basi, acha; tazama, nchi yote iko mbele yako; palipo pema machoni pako na pa kukufaa, nenda huko. 5#2 Fal 25:22; Mwa; 39:1; Yos 15:38; 1 Sam 2:30; Mit 15:16; Mt 6:33; Mdo 22:24,27,28 Alipokuwa bado hajaenda, akasema, Rudi sasa kwa Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa mtawala juu ya miji ya Yuda, ukakae pamoja naye kati ya watu; au nenda popote utakapoona mwenyewe kuwa pakufaa. Basi, mkuu wa askari walinzi akampa vyakula na zawadi, akamwacha aende zake. 6#Yer 39:14; Amu 20:1; 1 Sam 7:5,6 Basi, Yeremia akaenda kwa Gedalia, mwana wa Ahikamu, huko Mizpa, akakaa pamoja naye kati ya watu wale waliosalia katika nchi.
7 # 2 Fal 25:22-24; Yer 39:10 Kisha, wakuu wote wa majeshi waliokuwa katika bara, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, kuwa mtawala juu ya nchi, na kwamba amemkabidhi wanaume na wanawake na watoto, na baadhi ya maskini wa nchi wasiochukuliwa mateka Babeli; 8#Yer 41:1 ndipo wakamwendea Gedalia huko Mizpa; nao ni hawa, Ishmaeli, mwana wa Nethania, na Yohana na Yonathani, wana wa Karea, na Seraya, mwana wa Tanhumethi, na wana wa Efai, Mnetofa, na Yezania, mwana wa Mmaaka, wao na watu wao. 9Na Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, akawaapia wao na watu wao, akisema, Msiogope kuwatumikia Wakaldayo; kaeni katika nchi, mkamtumikie mfalme wa Babeli; nayo itawafaa. 10#Kum 16:13 Na mimi, tazama, nitakaa Mizpa, ili nisimame mbele ya Wakaldayo watakaotujia; lakini ninyi chumeni divai, na matunda ya wakati wa jua, na mafuta, mkaviweke vitu hivyo katika vyombo vyenu, mkakae katika miji yenu mliyoitwaa. 11#Isa 16:4; Yer 24:9; Omb 1:14 Kadhalika waliposikia Wayahudi wote, waliokuwa katika Moabu, na kati ya wana wa Amoni, na hao waliokuwa katika Edomu, na hao waliokuwa katika nchi zote, ya kuwa mfalme wa Babeli amewaachia Yuda mabaki, na ya kuwa amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, juu yao; 12basi, Wayahudi wote wakarudi kutoka kila mahali walikofukuzwa wakaenda mpaka nchi ya Yuda, wakamwendea Gedalia huko Mizpa, wakakusanya divai, na matunda ya wakati wa jua mengi sana.
13Tena Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa majeshi ya barani, wakamwendea Gedalia huko Mizpa, 14#Yer 25:21; 41:10; Amo 1:13; Zek 1:15 wakamwambia, Je! Una habari wewe ya kuwa Baalisi, mfalme wa wana wa Amoni, amemtuma Ishmaeli mwana wa Nethania, akuue? Lakini Gedalia, mwana wa Ahikamu, hakusadiki neno hili. 15Basi, Yohana, mwana wa Karea, akamwambia Gedalia huko Mizpa kwa siri, akisema, Niache niende nikampige Ishmaeli, mwana wa Nethania, wala hapana mtu atakayejua jambo hili; kwa nini akuue wewe, hata wakatawanyike Wayahudi waliokukusanyikia, na mabaki ya Yuda wakaangamie? 16#1 Kor 13:5 Lakini Gedalia, mwana wa Ahikamu, akamwambia Yohana, mwana wa Karea, Usilitende jambo hili, maana unamsingizia Ishmaeli.

Currently Selected:

Yeremia 40: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Video for Yeremia 40