Yeremia 44
44
Shutuma kwa kuendelea kuabudu miungu
1 #
Kut 14:2; Hos 9:6; Yer 46:14; 43:7; Isa 19:13; 11:11 Neno lililomjia Yeremia, kuhusu Wayahudi wote waliokaa katika nchi ya Misri, waliokaa Migdoli, na Tapanesi, na Nofu, na katika nchi ya Pathrosi, kusema, 2#Law 26:32-34; Isa 6:11; Yer 9:11; Mik 3:12; Lk 13:35 BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ninyi mmeona mabaya yote niliyoleta juu ya Yerusalemu, na juu ya miji yote ya Yuda; na, tazama, ni ukiwa leo, wala hapana mtu akaaye ndani yake; 3#Yer 19:4; Kum 13:6 kwa sababu ya uovu wao, waliotenda ili kunikasirisha, kwa kuwa walikwenda kufukiza uvumba, na kuwatumikia miungu mingine, ambao hawakuwajua, wao, wala ninyi, wala baba zenu. 4#2 Nya 36:15; Yer 7:25 Tena nilituma kwenu watumishi wangu wote, manabii, nikiamka mapema na kuwatuma, nikisema, Basi ninyi; msilifanye chukizo hili linalochukiza. 5Lakini hawakusikiliza, wala hawakutega masikio yao, ili wageuke na kuacha uovu wao, wasifukizie uvumba miungu mingine. 6#Yer 42:18; 1 Kor 10:11 Kwa sababu hiyo ghadhabu yangu, na hasira yangu, zilimwagika, nazo ziliwaka katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, na miji hiyo imeachwa ukiwa, na kuharibika, kama ilivyo leo. 7#Hes 16:38; Yer 7:19 Basi, sasa, BWANA, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kwa nini mnafanya uovu huu mkubwa juu ya nafsi zenu wenyewe, kujikatilia mbali mwanamume na mwanamke, mtoto mchanga na anyonyaye, mtoke kati ya Yuda, msijiachie mtu abakiye; 8#Yer 25:6,7; 42:18 kwa kuwa mnanikasirisha kwa matendo ya mikono yenu, mkifukizia uvumba miungu mingine katika nchi ya Misri, mlikokwenda kukaa ugenini; mpate kukatiliwa mbali, na kuwa laana, na aibu, katika mataifa yote ya dunia? 9Je! Mmeusahau uovu wa baba zenu, na uovu wa wafalme wa Yuda, na uovu wa wake zao, na uovu wenu wenyewe, na uovu wa wake zenu, walioutenda katika nchi ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu? 10#Mit 28:14 Hawajanyenyekea hata leo, wala hawakuogopa, wala hawakuenenda katika sheria yangu, wala katika amri zangu, nilizoweka mbele yenu, na mbele ya baba zenu. 11#Law 17:10; Yer 21:10; Amo 9:4 Basi, kwa sababu hiyo BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaelekeza uso wangu juu yenu, ili niwaletee mabaya, hata kukatilia mbali Yuda yote. 12#Kum 17:16; Isa 30:1-3; Yer 2:18; 18:16; 24:9; Mit 2:13,14; Zek 8:13 Nami nitawatwaa mabaki wa Yuda, walioelekeza nyuso zao kuiingia nchi ya Misri, wakae huko, nao wataangamia wote pia; wataanguka katika nchi ya Misri; wataangamia kwa upanga, na kwa njaa; watakufa, tangu wadogo hata wakubwa, kwa upanga, na kwa njaa; nao watakuwa apizo, na ajabu, na laana, na aibu. 13Kwa maana nitawaadhibu wakaao katika nchi ya Misri, kama nilivyouadhibu Yerusalemu, kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; 14hata katika watu wale wa Yuda waliosalia, waliokwenda nchi ya Misri ili wakae huko, hapatakuwa na mtu yeyote atakayepona, wala atakayesalia, na kupata kurudi nchi ya Yuda, ambayo wanatamani kurudi ili kukaa huko; maana hapana atakayerudi, ila wao watakaopona.
15Ndipo watu wote waliojua ya kuwa wake zao waliwafukizia uvumba miungu mingine, na wanawake wote waliosimama karibu, mkutano mkubwa, yaani, watu wote waliokaa katika nchi ya Misri, katika Pathrosi, wakamjibu Yeremia, wakisema, 16#Kut 5:12; Zab 2:3; Mit 1:24-27; Yer 6:16; Lk 19:14; Rum 2:3-9 Neno lile ulilotuambia kwa jina la BWANA, sisi hatutakusikiliza. 17#Hes 30:12; Kum 23:23; Amu 11:36 Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya. 18Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa. 19#Yer 7:18 Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimwandalia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mimiminiko, waume zetu wasipokuwapo? 20Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake, yaani, watu wote waliompa jibu lile, akisema, 21Uvumba mliofukiza katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, ninyi, na baba zenu, wafalme wenu, na wakuu wenu, na watu wa nchi, je! BWANA hakuwakumbuka watu hao? Je! Jambo hili halikuingia moyoni mwake? 22#Mwa 6:3; 19:13; 24:25; Isa 7:13; 43:24; Amo 2:13; Zab 107:33,34; Yer 25:11,18,38 Hata BWANA asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo. 23#Dan 9:11,12 Kwa sababu mmefukiza uvumba, na kwa sababu mmetenda dhambi juu ya BWANA, wala hamkuitii sauti ya BWANA, wala hamkwenda katika torati yake, wala katika amri zake, wala katika shuhuda yake; ndiyo maana mabaya haya yamewapata kama ilivyo leo.
24 #
Yer 43:7; 46:14 Tena Yeremia akawaambia watu wote, na wanawake wote, Lisikieni neno hili la BWANA, ninyi nyote wa Yuda, mlioko hapa katika nchi ya Misri; 25BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ninyi na wake zenu mmenena kwa vinywa vyenu, na kutimiza kwa mikono yenu, mkisema, Bila shaka tutazitimiza nadhiri zetu tulizoziweka, na kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji; basi, zithibitisheni nadhiri zenu, zitimizeni nadhiri zenu. 26#Mwa 22:16; Zab 50:16; Eze 20:39 Basi, kwa sababu hiyo lisikieni neno la BWANA, ninyi nyote wa Yuda, mnaokaa katika nchi ya Misri, Tazama, nimeapa kwa jina langu kuu, asema BWANA, ya kwamba jina langu halitatajwa tena katika kinywa cha mtu awaye yote wa Yuda, katika nchi yote ya Misri, akisema, Kama Bwana MUNGU aishivyo! 27#Yer 1:10; 2:17,19; 4:18; 5:19,29; 11:17; 31:38; Eze 7:6 Tazama, nawaangalia niwaletee mabaya, wala si mema; nao watu wote wa Yuda, walioko hapa katika nchi ya Misri, wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa, hadi wakomeshwe kabisa. 28#Law 26:44; Isa 27:13; Hab 3:2 Nao watakaoukimbia upanga, watatoka katika nchi ya Misri, na kuiingia katika nchi ya Yuda, watu wachache sana; na wote wa Yuda waliosalia, waliokwenda katika nchi ya Misri ili kukaa huko, watajua ni neno la nani litakalosimama, neno langu, au neno lao. 29#Zab 33:11 Na hii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu, asema BWANA, kwamba mimi nitawaadhibu ninyi mahali hapa, mpate kujua ya kuwa maneno yangu yatasimama juu yenu, kuwaletea mabaya bila shaka; 30#2 Fal 25:1-7; Yer 46:25,26; 39:5; Eze 29:3; Dan 4:35 BWANA asema hivi, Tazama, nitamtia Farao Hofra, mfalme wa Misri, katika mikono ya adui zake, na katika mikono yao wamtafutao roho yake; kama vile nilivyomtia Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mikono ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, adui yake aliyeitafuta roho yake.
Currently Selected:
Yeremia 44: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.