Yeremia 46
46
Hukumu juu ya Misri
1 #
Yer 25:15
Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, kuhusu mataifa. 2#2 Fal 23:29; 2 Nya 35:20; Yer 25:9,19 Kuhusu Misri; habari za jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri, lililokuwa karibu na mto Frati katika Karkemishi, ambalo Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alilipiga katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda.
3 #
Isa 8:9,10; Yer 51:11,12; Yoe 3:9,10; Nah 2:1 Tengenezeni kigao na ngao, mkakaribie ili kupigana. 4Watandikeni farasi; pandeni, enyi mpandao farasi; simameni na chapeo zenu, isugueni mikuki; zivaeni dirii. 5#Yer 6:25; 20:4; Ufu 6:15-17 Nimeyaona haya kwa sababu gani? Wamefadhaika, wamerudi nyuma; mashujaa wao wamevunjikavunjika; wanakimbia upesi sana, hawatazami nyuma; hofu iko pande zote; asema BWANA. 6#Dan 11:19 Mtu mwepesi asikimbie, wala shujaa asiokoke; pande za kaskazini karibu na mto Frati wamejikwaa na kuanguka.
7 #
Dan 11:22
Nani huyu ajiinuaye kama mto Nile,
Ambaye maji yake yanajirusha kama mito?
8Misri anajiinua kama mto Nile,
Na maji yake yanajirusha kama mito;
Asema, Nitajiinua, nitaifunika nchi;
Nitauharibu mji na hao wakaao ndani yake.
9Haya! Pandeni, enyi farasi;
Jihimizeni, enyi magari ya vita;
Mashujaa nao na watoke nje
Kushi na Puti, watumiao ngao;
Nao Waludi, washikao uta na kuupinda.
10 #
Yoe 1:15; Kum 32:42; Isa 34:6 Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi,
Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake;
Nao upanga utakula na kushiba,
Utakunywa damu yao hata kukinai;
Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yake
Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.
11 #
Yer 8:22; Isa 47:1 Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe. 12Mataifa wamesikia habari za aibu yako, nayo dunia imejaa kilio chako; maana shujaa amejikwaa juu ya shujaa mwenzake, wameanguka wote wawili pamoja.
Babeli itaivamia Misri
13 #
Yer 43:10-13; Isa 19:1; Eze 29:20 Neno hili ndilo ambalo BWANA alimwambia Yeremia, nabii, kueleza jinsi Nebukadneza, mfalme wa Babeli, atakavyokuja na kuipiga nchi ya Misri.
14Tangazeni habari hii katika Misri, mkaihubiri katika Migdoli, na kuihubiri katika Nofu, na Tapanesi; semeni, Simama, ujitayarishe kwa maana upanga umekula pande zako zote. 15Mbona mashujaa wako wamechukuliwa mbali? Hawakusimama kwa sababu BWANA aliwafukuza. 16#Law 26:37 Aliwakwaza wengi, naam, wakaangukiana wao kwa wao; wakasema, Haya! Na tuondoke, tukarudi kwa watu wetu wenyewe, hadi nchi tuliyozaliwa, tuukimbie upanga unaotuonea. 17Wakalia huko, Farao, mfalme wa Misri, ni kishindo tu; muda alioandikiwa ameuacha upite. 18#Isa 48:2; Mal 1:14; Yer 10:10; 44:26; 1 Tim 1:17; Hes 23:19 Kama mimi niishivyo, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi, hakika yake, kama Tabori katika milima, na kama Karmeli karibu na bahari, ndivyo atakavyokuja.
19 #
Yer 48:18
Ee binti ukaaye katika Misri,
Ujiweke tayari kwenda zako hali ya kufungwa;
Kwa maana Nofu utakuwa ukiwa,
Utateketezwa, usikaliwe na watu.
20 #
Hos 10:11; Yer 1:14 Misri ni mtamba mzuri sana, lakini uharibifu umekuja,
Umekuja utokao pande za kaskazini.
21Na askari wake waliojiwa, walio kati yake,
Ni kama ndama walionona malishoni;
Maana wao nao wamerudi nyuma,
Wamekimbia wote pamoja, wasisimame;
Maana siku ya msiba wao imewafikia,
Wakati wa kujiliwa kwao.
22 #
Isa 29:4
Sauti yake ni kama nyoka, wajapo kwa nguvu,
Watamjia na mashoka, kama wachanja kuni.
23Wataukata msitu wake, asema BWANA, ingawa haupenyeki;
Kwa maana ni wengi kuliko nzige, hawahesabiki.
24Binti ya Misri ataaibishwa;
Atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.
25 #
Eze 30:13
BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Amoni wa No, na Farao, na Misri, pamoja na miungu yake, na wafalme wake, naam, Farao, na hao wanaomtumainia; 26#Yer 44:30; 48:47; 49:39 nami nitawatia katika mikono ya hao wanaowatafuta roho zao, na katika mikono ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya watumishi wake; na baada ya hayo itakaliwa na watu, kama katika siku za kale, asema BWANA.
Mungu ataokoa Israeli
27 #
Yer 30:10-11; Isa 44:2 Lakini usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu. 28Usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema BWANA; kwa maana mimi ni pamoja nawe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokufukuza, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.
Currently Selected:
Yeremia 46: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.