YouVersion Logo
Search Icon

Ayubu 32

32
Elihu awakemea marafiki wa Ayubu
1Basi hao watu watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa sababu alikuwa mwenye haki machoni pake mwenyewe. 2#Mwa 22:21 Ndipo zikawaka hasira za huyo Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, katika jamaa ya Ramu, juu ya Ayubu, kwa sababu alikuwa amejipa haki mwenyewe zaidi ya Mungu. 3Tena hasira zake ziliwaka juu ya hao rafiki zake watatu kwa sababu hawakupata jawabu, lakini wamemhukumia Ayubu makosa. 4Basi huyo Elihu alikuwa anangoja ili anene na Ayubu, kwa sababu hao wengine walikuwa wazee kuliko yeye. 5Hata Elihu alipoona kuwa hapana jawabu katika vinywa vya watu hao watatu, hasira zake ziliwaka.
6Basi Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, akajibu, na kusema,
Mimi ni kijana, na ninyi ni wazee sana;
Kwa hiyo nilijizuia, nisithubutu kuwaonesha nionavyo.
7 # Ayu 8:8,9 Nilisema, Yafaa siku ziseme,
Na wingi wa miaka ufundishe hekima.
8 # 1 Fal 3:9 Lakini hakika imo roho ndani ya mwanadamu,
Na pumzi ya Mwenyezi ndiyo impayo ufahamu.
9 # 1 Kor 1:21 Sio wakuu walio wenye hekima,
Wala sio wazee watambuao haki.
10Basi nilisema, Nisikilizeni mimi;
Mimi nami nitawaonesha nionavyo.
11Tazama, niliyangojea maneno yenu,
Nilizisikiliza nisikie hoja zenu,
Hapo mlipokitafuta mtakalonena.
12 # Mit 18:13 Naam, niliwasikiza ninyi,
Na tazama, hapana mmoja aliyemshinda Ayubu,
Wala kumjibu maneno yake, kati yenu.
13 # Yer 9:23 Jitunzeni msiseme, Sisi tumepata hekima;
Mungu huenda akamshinda, si mtu;
14Kwa kuwa yeye hajayaelekeza maneno yake kwangu;
Wala sitamjibu mimi kwa maneno yenu.
15Wameshangaa, hawajibu tena;
Hawana neno la kusema.
16Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni,
Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena;
17Mimi nami nitajibu sehemu yangu,
Mimi nami nitaonesha nionavyo.
18Kwa kuwa nimejaa maneno;
Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.
19Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa;
Kama viriba vipya liko karibu kupasuka.
20Nitanena, ili nipate kutulia;
Nitafunua midomo yangu na kujibu.
21Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu;
Wala sitajipendekeza kwa mtu yeyote.
22 # Mdo 12:22,23 Kwa kuwa mimi sijui kujipendekeza;
Au Muumba wangu angeniondoa kwa upesi.

Currently Selected:

Ayubu 32: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in