YouVersion Logo
Search Icon

Ayubu 37

37
1Moyo wangu hutetemeka kwa hayo pia,
Nao huruka kutoka mahali pake.
2Zisikizeni hizo kelele za sauti yake,
Na uvumi utokao kinywani mwake.
3Yeye huituma iende chini ya mbingu zote,
Na radi yake hata miisho ya nchi.
4Baadaye sauti hunguruma;
Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake;
Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.
5Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake;
Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuyaelewa.
6Kwa kuwa huiambia theluji, Anguka juu ya nchi;
Na pia kwa manyunyu ya mvua,
Hayo manyunyu ya mvua yake nyingi.
7 # Zab 111:2 Huufunga mkono wa kila binadamu;
Ili watu wote aliowaumba wajue.
8Hapo wanyama huingia mafichoni,
Na kukaa katika mapango yao.
9Dhoruba hutoka katika vyumba vyake;
Na baridi ghalani mwake.
10Kwa pumzi ya Mungu barafu hutokea;
Na uso wa maji huganda punde.
11Naam, huyatwika mawingu mazito mzigo wa maji;
Hulitandika wingu la umeme wake;
12Nalo hugeuzwa huku na huku kwa uongozi wake,
Ili yafanye yote atakayoyaagiza
Juu ya uso wa dunia hii ikaayo watu;
13Kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake,
Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye.
14Sikiliza neno hili, Ee Ayubu;
Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu.
15Je! Wajua wewe jinsi Mungu anavyoziagiza,
Na kuufanya umeme wa wingu lake uangaze?
16 # Ayu 36:4 Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa,
Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?
17Jinsi nguo zako zilivyo na moto,
Hapo nchi ituliapo kwa sababu ya upepo wa kusini?
18 # Mwa 1:6; Ayu 37:11-18 Je! Waweza kuzitandaza mbingu pamoja naye,
Ambazo zina nguvu kama kioo cha kuyeyushwa?
19Utufundishe ni maneno gani tutakayomwambia;
Kwa kuwa hatuwezi kutoa hoja zetu maana tumo gizani.
20Je! Aambiwe kwamba nataka kunena?
Au kuna mtu ambaye angetamani kumezwa?
21Na sasa watu hawawezi kuutazama mwanga ung'aao mbinguni;
Lakini upepo ukipita huzitakasa.
22Kaskazini hutokea mng'ao wa dhahabu;
Mungu huvikwa ukuu utishao.
23 # Kut 33:20; Mt 11:27; Yn 1:18; Ayu 36:5; Zab 99:4; Yer 10:12; Omb 3:33; Ebr 12:10 Yeye Mwenyezi hamwezi kumwona;
Yeye ni mkuu mwenye uweza;
Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.
24 # Mt 10:28; 11:25 Kwa hiyo watu humwogopa;
Yeye hawaangalii walio na hekima mioyoni.

Currently Selected:

Ayubu 37: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in