YouVersion Logo
Search Icon

Yoshua UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu hiki cha Yoshua kimepewa jina la mtu aliyerithi uongozi kutoka kwa Musa (Hesabu 27:18-23). Yoshua ni wa kabila la Efraimu. Waisraeli walipotoka Misri alikuwa bado kijana. Safarini jangwani Musa alimteua kuwa kiongozi (Kut 17:8-16; 33:11; Hes 13:8,16). Yamkinika Yoshua alianza kuwaongoza Waisraeli akiwa na umri wa miaka kati ya 70 na 80. Alikufa akiwa na umri wa miaka 110, akazikwa Timnath-sera kwenye milima ya Efraimu (24:29-30). Yoshua anahesabiwa kuwa kiongozi hodari, shujaa na mcha Mungu. Aliamini kuwa mafanikio yao hayatokani na kutegemea nguvu na uhodari wa jeshi lao bali utii mkamilifu kwa Agano lao na Mungu.
Kitabu cha Yoshua kinaendeleza masimulizi ya kitabu cha Hesabu, kwa kuanzia pale kitabu cha Hesabu kilipoishia. Aidha kina mkazo maalumu juu ya historia ya wokovu. Mungu alichagua taifa la Israeli; pia ana wivu kwa taifa lake, anataka limtumikie yeye tu (21:43-45; 23:11; 24:14).
Kinasimulia juu ya Waisraeli kuvuka Yordani, kushambulia, kushinda na kuteka nchi ya Kanaani, kugawanya nchi hiyo katika makabila ya Waisraeli na kuweka miji maalumu kwa wakimbizi vinatokana na uaminifu na utendaji wa Mungu. Kabla ya kufa kwake, Yoshua anakumbusha kuwa hawana budi kumtii Mungu na Agano lake.
Yaliyomo:
1. Waisraeli waiteka Kanaani, Sura 1-12
2. Kugawana nchi ya Kanaani, Sura 13-21
3. Kurudi kwa makabila ya mashariki, Sura 22
4. Hotuba ya mwisho ya Yoshua, Sura 23
5. Agano la kumtumikia Mungu, Sura 24:1-28
6. Kifo na mazishi ya Yoshua na Eleazari, Sura 24:29-33

Currently Selected:

Yoshua UTANGULIZI: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in