YouVersion Logo
Search Icon

Mika 1

1
1 # 2 Pet 1:21; Yer 26:18; 2 Fal 15:32—16:20; 18:1—20:21; 2 Nya 27:1-7; 28:1—32:33 Hili ndilo neno la BWANA lililomjia Mika, Mmoreshathi, katika siku za Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; maono aliyoyaona kuhusu Samaria na Yerusalemu.
Hukumu yatangazwa juu ya Samaria
2Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu. 3#Isa 26:21; Eze 3:12; Ebr 12:18,19 Kwa maana, angalieni, BWANA anakuja akitoka mahali pake, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka. 4Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika katika mteremko. 5#Yer 2:18,19; Hos 5:5 Kwa sababu ya kosa la Yakobo yametokea haya yote, na kwa sababu ya makosa ya nyumba ya Israeli. Nini kosa la Yakobo? Je, silo Samaria? Na nini mahali pa Yuda palipoinuka? Sipo Yerusalemu? 6#2 Fal 19:25 Kwa ajili ya hayo nitafanya Samaria kuwa kama chungu katika shamba, na kama miche ya shamba la mizabibu; nami nitayatupa mawe yake bondeni, nami nitaifunua misingi yake. 7Na sanamu zake zote za kuchonga zitapondwapondwa, na ijara zake zote zitateketezwa kwa moto, na sanamu zake zote nitazifanya ukiwa; kwa kuwa amezikusanya kwa ujira wa kahaba, nazo zitaurudia ujira wa kahaba.
Maangamizi ya miji ya Yuda
8Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia,
Nitakwenda nimevua nguo, nikiwa uchi;
Nitaomboleza kama mbweha,
Na kulia kama mbuni.
9 # 2 Fal 18:13 Kwa maana majeraha yake hayaponyeki;
Maana msiba umeijia hata Yuda,
Unalifikia lango la watu wangu,
Naam, hata Yerusalemu.
10Msiyahubiri haya katika Gathi, msilie kamwe;
Katika Beth-le-Afra ugaegae mavumbini.
11Piteni; njia yenu, wakazi wa Shafiri, mkiwa uchi na wenye aibu;
Wakazi wa Saanani msitokeze nje;
Beth-eseli unalia
na ataondoa msaada wake kwenu;
12Maana wakazi wa Marothi wanasubiri kwa hamu kupata mema;
Lakini maangamizi yameshuka toka kwa BWANA,
Yamefika katika lango la Yerusalemu.
13Mfungie gari la vita farasi
Aliye mwepesi, wakazi wa Lakishi;
Alikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni;
Maana makosa ya Israeli yameonekana kwako.
14Kwa hiyo mtaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia;
Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli.
15Bado, wakazi wa Maresha, nitawaleteeni tena yeye atakayewamiliki;
Utukufu wa Israeli utafika Adulamu.
16 # 2 Fal 17:6 Jinyoeni upara, jikateni nywele zenu,
Kwa ajili ya watoto waliowafurahisha;
Panueni upara wenu kama tai;
Kwa maana wamekwenda mbali nanyi uhamishoni.

Currently Selected:

Mika 1: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Video for Mika 1