YouVersion Logo
Search Icon

Hesabu 32

32
Ushindi na mgawanyo wa Kanaani
1 # Hes 21:32; Yos 13:25; 2 Sam 24:5; Isa 16:8,9 Basi wana wa Reubeni, na hao wana wa Gadi, walikuwa na wanyama wa mifugo wengi sana; nao walipoona nchi ya Yazeri, na nchi ya Gileadi, ya kuwa mahali hapo palikuwa ni mahali pa kuwafaa wanyama; 2hao wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, wakamwendea Musa na Eleazari kuhani, na wakuu wa mkutano, wakanena nao, wakisema, 3Atarothi, na Diboni, na Yazeri, na Nimra, na Heshboni, na Eleale, na Sebamu, na Nebo na Beoni, 4#Hes 21:24,34 nchi hiyo ambayo BWANA aliipiga mbele ya mkutano wa Israeli, ni nchi ifaayo kwa mifugo, nasi watumishi wako tunayo mifugo. 5Wakasema, Kama tumepata kibali mbele ya macho yako, sisi watumishi wako na tupewe nchi hii iwe milki yetu; usituvushe mto wa Yordani. 6Musa akawaambia wana wa Gadi na wana wa Reubeni, Je! Ndugu zenu waende vitani nanyi mtaketi hapa? 7Mbona mwawavunja mioyo yao wana wa Israeli, wasivuke na kuingia nchi hiyo ambayo BWANA amewapa? 8#Hes 13:3,17-33; Kum 1:22 Ndivyo walivyofanya baba zenu, hapo nilipowatuma kutoka Kadesh-barnea ili waende kuiangalia hiyo nchi. 9#Hes 1:10; 13:24,31; Kum 1:24 Kwa kuwa walipokwea na kuingia bonde la Eshkoli, na kuiona nchi, wakawavunja mioyo wana wa Israeli, ili wasikwee kuingia nchi aliyowapa BWANA. 10#Hes 14:11; Kum 1:34; Zab 95:11; Eze 20:15; Ebr 3:8-19 Na siku ile hasira za BWANA ziliwaka, naye akaapa, akisema, 11#Kum 1:35; Hes 14:24 Hakika yangu hapana mtu mmoja katika wale watu waliotoka Misri, tangu huyo aliyepata umri wa miaka ishirini, na zaidi, atakayeiona hiyo nchi niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; kwa sababu hawakuniandama kwa moyo wote; 12#Kum 1:36; Yos 14:8,9; Ayu 4:7; Zab 37:29; Mit 11:31 ila Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni; kwa kuwa wao wamemwandama BWANA kwa moyo wote. 13#Hes 14:33; 26:64 Na hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, naye akawatembeza huku na huko jangwani muda wa miaka arubaini, hata kizazi hicho kizima kilichokuwa kimefanya uovu machoni pa BWANA kilipoisha angamia. 14#Kum 1:34 Na tazama, ninyi kizazi cha watu wenye dhambi, mmeinuka badala ya baba zenu ili kuongeza tena hizo hasira kali za BWANA juu ya Israeli. 15#Kum 30:17; Yos 22:16,18; 2 Nya 7:19; 15:2 Kwa kuwa mkigeuka msimfuate, yeye atawaacha tena nyikani; nanyi mtawaangamiza watu hawa wote. 16Basi wakamwendea karibu, na kusema, Sisi tutafanya mazizi hapa kwa ajili ya mifugo yetu, na kujenga miji kwa ajili ya watoto wetu; 17#Yos 4:12,13 lakini sisi wenyewe tutakuwa tayari na silaha zetu kutangulia mbele#32:17 Katika Kiebrania ni ‘kuharakisha mbele’. ya wana wa Israeli, hata tutakapowafikisha mahali pao; na watoto wetu watakaa katika hiyo miji yenye maboma, kwa sababu ya wenyeji wa nchi. 18#Yos 22:4 Sisi hatutarudia nyumba zetu, hata wana wa Israeli watakapokuwa wamekwisha kurithi kila mtu urithi wake. 19#Yos 12:1; 13:8 Kwa kuwa sisi hatutarithi pamoja nao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, huko mbele; kwa sababu urithi wetu umetuangukia upande huu wa Yordani mwa mashariki. 20#Kum 3:18; Yos 1:14; 4:12,13 Basi Musa akawaambia, Kama mtafanya jambo hili; kama mtajivika silaha, ili kutangulia mbele ya BWANA mwende vitani, 21tena kama kila mume wa kwenu mwenye kuchukua silaha atavuka Yordani mbele ya BWANA, hata atakapokuwa amekwisha watoa adui zake mbele yake, 22#Kum 3:20; Yos 11:23; 18:1; 22:4,9; Kum 3:12; Yos 1:15; 13:8,32 na hiyo nchi kushindwa mbele za BWANA; ndipo baadaye mtarudi, nanyi mtakuwa hamna hatia mbele za BWANA, wala kwa Israeli; na nchi hii itakuwa milki yenu mbele za BWANA. 23#Mwa 4:7; 44:16; Zab 140:11; Mit 13:21; Isa 3:11; 59:12; Rum 2:9; 1 Kor 4:5 Lakini kama hamtaki kufanya neno hilo, ninyi mmefanya dhambi mbele za BWANA, nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata, hapana budi. 24#Hes 32:16,34 Basi, jengeni miji kwa ajili ya watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya kondoo zenu; mkayafanye hayo mliotamka kwa vinywa vyenu. 25Ndipo wana wa Gadi na wana wa Reubeni wakanena na Musa, na kumwambia, Sisi watumishi wako tutafanya kama wewe bwana wangu utuagizavyo. 26#Yos 1:14 Watoto wetu, na wake wetu, na kondoo wetu, na ng'ombe wetu wote, watakuwa hapo katika miji ya Gileadi; 27#Yos 4:12 lakini sisi watumishi wako tutavuka, kila mwanamume aliyevaa silaha za vita, mbele za BWANA, tuende vitani, kama wewe bwana wangu usemavyo.
28 # Yos 1:12-15 Basi Musa akamwagiza Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na wakuu wa nyumba za mababa za makabila ya wana wa Israeli, kuhusu watu hao. 29Musa akawaambia, Kwamba wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, watavuka Yordani pamoja nanyi, kila mtu akiwa amevaa silaha kwa vita, mbele za BWANA, nayo nchi itashindwa mbele yenu; ndipo mtawapa nchi ya Gileadi kuwa milki yao; 30lakini ikiwa hawataki kuvuka pamoja nanyi, wakiwa wamevaa silaha zao, ndipo watakuwa na milki zao kati yenu katika nchi ya Kanaani. 31Wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, wakajibu na kusema, Kama BWANA alivyotuambia sisi watumishi wako, ndivyo tutakavyofanya. 32Tutavuka, tukiwa tumevaa silaha zetu, mbele za BWANA, kuingia nchi ya Kanaani, nayo milki ya urithi wetu itakuwa ng'ambo ya pili#32:32 au ‘katika upande huu wa Yordani’. ya Yordani. 33#Kum 3:12; Yos 12:6; 13:8; 22:4; Hes 21:24; Kum 2:30-35; 3:1-8; Zab 135:10,11; 136:18 Basi Musa akawapa wao, maana, wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, na hiyo nusu ya kabila la Manase, mwana wa Yusufu, ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, hiyo nchi, kama miji yao ilivyokuwa, pamoja na mipaka yake, maana, miji ya hiyo nchi iliyozunguka kotekote. 34#Hes 33:45; Kum 2:36 Kisha wana wa Gadi wakajenga Diboni, na Atarothi, na Aroeri; 35na Atrothi-shofani, na Yazeri, na Yogbeha; 36na, Beth-nimra, na Beth-harani; miji yenye maboma, na mazizi ya kondoo. 37Na wana wa Reubeni wakajenga Heshboni, na Eleale, na Kiriathaimu; 38#Isa 46:1; Hes 22:41; Kut 23:13 na Nebo, na Baal-meoni, (majina yake yalikuwa yamegeuzwa) na Sibma; nao wakaiita miji waliyoijenga majina mengine. 39#Mwa 50:23; Hes 26:29; Yos 17:1 Na wana wa Makiri mwana wa Manase wakaenda Gileadi, na kuitwaa, na kuwapokonya Waamori waliokuwa humo. 40#Kum 3:12; Yos 17:1 Basi Musa akampa Makiri, mwana wa Manase, Gileadi, naye akakaa humo. 41#Kum 3:14; Yos 13:30; 1 Nya 2:21; Amu 10:4; 1 Fal 4:13 Kisha Yairi mwana wa Manase akaenda na kuvitwaa vijiji vya Gileadi. Akaviita jina lake Hawoth-yairi.#32:41 Katika Kiebrania ni ‘vijiji vya Yairi’. 42#2 Sam 18:18; Zab 49:11 Kisha Noba akaenda na kutwaa Kenathi na vijiji vyake, na kuita jina lake Noba, kwa kuandama jina lake mwenyewe.

Currently Selected:

Hesabu 32: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in