YouVersion Logo
Search Icon

Hesabu 35

35
Miji kwa makuhani
1 # Yos 21:1-42 Kisha BWANA akanena na Musa katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko, akamwambia, 2#Law 25:32,33; Hes 18:20-24; Kum 18:1,2; 1 Nya 6:64; Yos 14:3,4; 21:2; Eze 45:1; 48:8 Uwaagize wana wa Israeli wawape Walawi miji wapate mahali pa kukaa, katika milki yao; pamoja na malisho yaliyoizunguka hiyo miji kotekote mtawapa Walawi. 3Hiyo miji watakuwa nayo ili wakae humo, na malisho watakuwa nayo kwa wanyama wao wa mifugo, na kwa mali zao, na kwa wanyama wao wote. 4Na yale malisho ya miji mtakayowapa Walawi, ukubwa wake utakuwa tangu ukuta wa mji kupima kiasi cha dhiraa elfu pande zote. 5Nanyi mtapima hapo nje ya mji upande wa mashariki dhiraa elfu mbili, na upande wa kusini dhiraa elfu mbili, na upande wa magharibi dhiraa elfu mbili, na upande wa kaskazini dhiraa elfu mbili, huo mji ulio katikati. Hayo ndiyo yatakayokuwa kwao malisho ya miji. 6#Kum 4:41; Yos 20:2; 21:3; Zab 9:9; 62:7,8; Isa 4:6 Na hiyo miji mtakayowapa Walawi, itakuwa miji sita ya kukimbilia, mtakayoweka kwa ajili ya mwenye kumwua mtu, ili akimbilie huko; pamoja na hiyo mtawapa miji arubaini na miwili zaidi. 7#1 Nya 6:54-81; Yos 21:41 Miji yote mtakayowapa hao Walawi jumla yake itakuwa miji arubaini na minane; mtawapa miji hiyo pamoja na malisho yake. 8#Yos 21:3; Kut 16:18; Hes 26:54; 33:54 Tena katika miji mtakayotoa ya hiyo milki ya wana wa Israeli, katika hao walio wengi mtatwaa miji mingi; na katika hao walio wachache mtatwaa miji michache; kila mtu kama ulivyo urithi wake atakaourithi, atawapa Walawi katika miji yake.
Miji ya makimbilio
9 # Kum 19:2-4; Yos 20:1-9 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 10#Kum 19:2; Yos 20:2 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani, 11#Kut 21:13 Ndipo mtajiwekea miji itakayokuwa ya makimbilio kwa ajili yenu; ili kwamba mwenye kumwua mtu, pasipo kukusudia kumwua, apate kukimbilia huko. 12#Kum 19:6; Yos 20:3 Na hiyo miji itakuwa kwenu kuwa makimbilio, kumkimbia mwenye kulipiza kisasi, ili asiuawe mwenye kumwua mtu, hata atakaposimama mbele ya mkutano ahukumiwe. 13Na hiyo miji mtakayowapa itakuwa kwenu ni miji sita ya kukimbilia. 14#Kum 4:41; 2 Kor 8:13,14 Mtawapa miji mitatu ng'ambo ya pili ya Yordani, na miji mitatu mtawapa katika nchi ya Kanaani; miji hiyo itakuwa ni miji ya makimbilio. 15#Hes 15:16 Miji hiyo sita itakuwa pa kukimbilia usalama kwa ajili ya wana wa Israeli, kwa ajili ya mgeni na kwa ajili ya aishiye nao kama mgeni; ili kila amwuaye mtu, bila kukusudia kuua, apate mahali pa kukimbilia.
Kuhusu kuua na kulipiza kisasi cha damu
16 # Kut 21:12,14; Law 24:17; Kum 19:11,12 Lakini kama alimpiga kwa chombo cha chuma, akafa, ni mwuaji huyo; mwuaji hakika yake atauawa. 17Na kama alimpiga kwa jiwe lililokuwa mkononi mwake, ambalo kwa hilo humkini mtu kufa, naye akafa, yeye ni mwuaji; huyo mwuaji lazima atauawa. 18Au kama alimpiga kwa chombo cha mti kilichokuwa mkononi mwake ambacho kwa hicho humkini mtu kufa, naye akafa, ni mwuaji huyo, mwuaji lazima atauawa. 19Mwenye kutwaa kisasi cha damu ndiye atakayemwua mwuaji; hapo atakapokutana naye, atamwua. 20#Mwa 4:8; 2 Sam 3:27; 20:10; 1 Fal 2:31; Lk 4:29; Kut 21:14; Kum 19:11; 1 Sam 18:10,11,25; 20:1; 23:7,8; Zab 10:7-10; 30:7,8 Tena kama alimsukuma kwa kumchukia au kama alimtupia kitu kwa kumvizia, hadi akafa; 21au akampiga kwa mkono wake kwa kuwa ni adui, naye akafa; yeye aliyempiga lazima atauawa; yeye ni mwuaji; mwenye kutwaa kisasi cha damu atamwua mwuaji, hapo atakapokutana naye. 22Lakini ikiwa alimsukuma ghafla pasipo kumchukia; au akamtupia kitu chochote pasipo kumvizia, 23au kwa jiwe liwalo lote, ambalo kwa kupigwa kwalo humkini mtu kufa, bila kumwona#35:23 au ‘bila, kukusudia’. akamtupia hata akafa, naye hakuwa adui yake, wala hakumtakia madhara; 24#Yos 20:6 ndipo mkutano utaamua kati ya huyo aliyempiga mtu na huyo atakayelipiza kisasi cha damu, kama hukumu hizi zilivyo; 25#Efe 1:7; Kut 29:7; Law 4:3; 21:10 nao mkutano utamwokoa yule aliyemwua mtu na mkono wa mwenye kulipiza kisasi cha damu; tena mkutano utamrejesha katika mji wake wa makimbilio, aliokuwa anaukimbilia; naye atakaa humo hata kifo chake kuhani mkuu, aliyepakwa mafuta matakatifu. 26Lakini kama mwenye kumwua mtu akienda wakati wowote kupita mpaka wa huo mji wa makimbilio, alioukimbilia; 27#Kut 22:2 na mwenye kutwaa kisasi cha damu akamwona, naye yuko nje ya mpaka wa mji wake wa makimbilio, na mwenye kutwaa kisasi cha damu akamwua huyo mwuaji, hatakuwa na hatia ya damu; 28kwa sababu ilimpasa kukaa ndani ya mji wake wa makimbilio hadi kifo chake kuhani mkuu lakini kuhani mkuu atakapokwisha kufa huyo mwuaji atarudi aende nchi ya urithi wake. 29#Hes 27:11 Mambo haya yatakuwa ni amri ya hukumu kwenu, katika vizazi vyenu vyote, katika makazi yenu yote. 30#Kum 17:6; 19:15; Mt 18:16; 2 Kor 13:1; 1 Tim 5:19; Ebr 10:28; Ufu 11:3 Mtu yeyote atakayemwua mtu, huyo mwuaji atauawa kwa vinywa vya mashahidi; lakini shahidi mmoja hatashuhudia juu ya mtu akauliwa. 31Tena, msipokee fidia kwa ajili ya uhai wa mwuaji, ambaye amekuwa na hatia ya mauti; Lakini lazima atauawa. 32#Mdo 4:12; Gal 2:21 Tena hamtapokea fidia kwa ajili ya huyo aliyeukimbilia mji wake wa makimbilio, apate kwenda tena kukaa katika nchi, hata kifo cha kuhani mkuu. 33#Mwa 4:9-12; Law 18:25; Kum 21:23; Zab 106:38; Isa 26:21; Hos 4:2,3; Mik 4:11; Mwa 9:6 Hivi hamtaitia unajisi nchi ambayo mwakaa; kwa kuwa damu huitia nchi unajisi; wala hapana sadaka itoshayo kwa ajili ya nchi, kwa ajili ya damu iliyomwagwa ndani yake, isipokuwa ni damu ya huyo aliyeimwaga. 34#Law 18:25; Kum 21:23; Kut 29:45,46; Hes 5:3; Zab 76:2; Isa 8:18; Hos 9:3; 2 Kor 6:16 Kwa hiyo msiitie unajisi nchi mwishiyo ambayo nami nakaa kati yake; kwa kuwa mimi BWANA nakaa kati ya wana wa Israeli.

Currently Selected:

Hesabu 35: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in