YouVersion Logo
Search Icon

Hesabu 36

36
Wanawake walioolewa na urithi wao
1 # Hes 26:29 Kisha wale wakuu wa nyumba za mababa ya jamaa ya wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, katika jamaa za wana wa Yusufu, wakakaribia, na kunena mbele ya Musa, na mbele ya wakuu walio juu ya nyumba za mababa ya wana wa Israeli; 2#Hes 27:1,7; 26:55; 33:54; Yos 17:3,4 wakasema, BWANA alimwagiza bwana wangu awape wana wa Israeli nchi kwa kupiga kura iwe urithi wao; tena bwana wangu aliagizwa na BWANA awape binti za Selofehadi ndugu yetu huo urithi wa baba yao. 3Wakiolewa na watu wa wana wa hayo makabila mengine ya wana wa Israeli, ndipo urithi wao utatwaliwa na kuondolewa katika urithi wa baba zetu, na hilo kabila watakalotiwa ndani yake litaongezewa urithi wao; basi urithi huo utaondolewa katika kura ya urithi wetu. 4#Law 25:10 Tena itakapokuwapo hiyo jubilii ya wana wa Israeli, ndipo urithi wa hilo kabila ambalo wamekuwa ndani yake utaongezewa huo urithi wao; hivyo urithi wao utaondolewa katika urithi wa kabila la baba zetu. 5#Hes 27:7 Basi Musa akawaagiza wana wa Israeli kama neno la BWANA lilivyokuwa, akasema, Kabila la wana wa Yusufu imenena yaliyo haki. 6BWANA ameagiza neno hili katika habari ya binti za Selofehadi, akasema, Na waolewe na waume wawapendao; lakini na waolewe katika jamaa ya kabila la baba zao. 7#1 Fal 21:3 Hivyo hapana urithi wowote wa wana wa Israeli utakaotoka kabila hili kwenda kabila hili; kwa kuwa wana wa Israeli watashikamana kila mtu na urithi wa kabila la baba zake. 8#1 Nya 23:22 Na kila binti atakayemiliki urithi katika kabila lolote katika wana wa Israeli, ataolewa katika jamaa moja ya kabila la baba yake, ili wana wa Israeli wapate kumiliki kila mtu urithi wa baba zake. 9Hivyo hapatakuwa na urithi wowote utakaotoka kabila hili kwenda kabila hili; kwa kuwa makabila ya wana wa Israeli yatashikamana kila mmoja na urithi wake mwenyewe. 10Basi hao binti za Selofehadi wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa; 11#Hes 27:1 kwa kuwa Mala, na Tirza, na Hogla, na Milka, na Nuhu, binti za Selofehadi waliolewa na wanaume, wana wa ndugu za baba yao. 12Waliolewa katika jamaa za wana wa Manase, mwana wa Yusufu, na urithi wao ukakaa katika kabila la jamaa ya baba yao.
13 # Hes 22:1; 26:3; 31:12; 33:50; Kum 33:4; Neh 9:12-14; Yn 1:17; 7:19 Haya ndiyo maagizo na hukumu, ambayo BWANA aliwaagiza wana wa Israeli, kwa mkono wa Musa, hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko.

Currently Selected:

Hesabu 36: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in