Mithali 17
17
1Afadhali mego kavu pamoja na utulivu,
Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.
2Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu;
Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.
3 #
Zab 26:2; Mit 27:21; Yer 17:10; Mal 3:3 Kalibu ni kwa fedha, na tanuri kwa dhahabu;
Bali BWANA huijaribu mioyo.
4Mtenda mabaya husikiliza midomo ya uovu;
Na mwongo hutega sikio lake kusikiliza ulimi wa madhara.
5 #
Ayu 31:29; Mit 24:17; Oba 1:12 Amchekaye maskini humtukana Muumba wake;
Naye aufurahiaye msiba hatakosa adhabu.
6Wana wa wana ndio taji la wazee,
Na utukufu wa watoto ni baba zao.
7Maneno mazuri hayapendezi kinywani mwa mpumbavu;
Sembuse midomo ya uongo kinywani mwa mkuu.
8 #
Mwa 39:21; Dan 6:3 Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho;
Kila kigeukapo hufanikiwa.
9Afunikaye kosa hutafuta kupendwa;
Bali yeye afichuaye siri hutenga rafiki.
10Lawama hupenya moyoni mwa mwenye ufahamu,
Kuliko mapigo mia moyoni mwa mpumbavu.
11Mtu mwovu hataki neno ila kuasi tu;
Kwa hiyo mjumbe mkali atatumwa kwake.
12Afadhali mtu akutwe na dubu jike aliyenyang'anywa watoto wake,
Kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake.
13 #
Yer 18:20; Rum 12:17; 1 The 5:15 Yeye arudishaye mabaya badala ya mema,
Mabaya hayataondoka nyumbani mwake.
14 #
Mit 20:3; Mdo 6:1; Rum 12:18; 1 The 4:11 Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji;
Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.
15 #
Kut 23:7; Isa 5:23 Yeye asemaye kwamba asiye haki ana haki;
naye asemaye kwamba mwenye haki hana haki;
Hao wote wawili ni chukizo kwa BWANA.
16Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima,
Ikiwa hana moyo wa ufahamu?
17Rafiki hupenda sikuzote;
Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.
18Asiye na hekima hupeana mkono na mtu;
Na kuwa mdhamini wa mtu mwingine.
19Apendaye ugomvi hupenda dhambi;
Auinuaye sana mlango wake hutafuta uharibifu.
20Mtu mwenye moyo wa ukaidi hatapata mema;
Na mwenye ulimi wa upotovu huanguka katika misiba.
21Azaaye mpumbavu ni kwa huzuni yake mwenyewe;
Wala baba wa mpumbavu hana furaha.
22Moyo uliochangamka ni dawa nzuri;
Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.
23 #
Kut 23:8
Asiye haki hutoa rushwa kifuani,
Ili kuzipotosha njia za hukumu.
24 #
Mhu 2:14
Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu;
Bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia.
25Mwana mpumbavu ni huzuni kwa babaye,
Na uchungu kwa mamaye aliyemzaa.
26Tena kumwadhibu mwenye haki si vizuri;
Wala si vyema kuwapiga wakuu kwa unyofu wao.
27 #
Yak 1:19
Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa;
Na mwenye roho ya utulivu ana busara.
28Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima;
Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.
Currently Selected:
Mithali 17: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.