Zaburi 144
144
Sala kwa ukombozi wa kitaifa na usalama
Ya Daudi.
1 #
2 Sam 22:35
Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu,
Aifundishaye mikono yangu vita,
Na vidole vyangu kupigana.
2Mwamba#144:2 Au Mhisani. wangu na ngome yangu,
Nguzo yangu na mwokozi wangu
Ngao yangu ninayemkimbilia,
Huwatiisha watu wangu chini yangu.
3 #
Ayu 7:17-18; Zab 8:4; Ebr 2:6 Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjali?
Na binadamu hata umwangalie?
4Binadamu ni kama ubatili,
Siku zake ni kama kivuli kipitacho.
5 #
Isa 64:1
Ee BWANA, uziinamishe mbingu zako, ushuke chini.
Uiguse milima ili nayo itoe moshi.
6Utupe umeme, uwatawanye,
Uipige mishale yako, uwafadhaishe.
7 #
Zab 69:1; Mal 2:11 Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye,
Unitoe katika maji mengi, kutoka kwa mkono wa wageni,
8Vinywa vyao vinasema visivyofaa,
Na ambao mikono yao ya kulia ni ya uongo.
9 #
Zab 33:2
Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,
Kwa kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.
10Awapaye wafalme wokovu,
Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.
11Uniponye, unitoe,
Katika mkono wa wageni.
Vinywa vyao vyasema visivyofaa,
Na mkono wao wa kulia ni mkono wa uongo.
12Wavulana wetu wakiwa ujanani wawe kama miche
Iliyostawi kikamilifu.
Binti zetu wawe kama nguzo za pembeni
Zilizochongwa#144:12 au zilizonakishiwa. ili kupamba kasri.#144:12 au hekalu.
13Ghala zetu na zijae
Zenye akiba za jinsi zote.
Kondoo zetu na wazae
Elfu na makumi elfu mashambani mwetu.
14 #
Law 26:17
Ng'ombe wetu na wabebe mizigo mizito,
Kusiwe na kushambuliwa.
Wala kusiwe na kuhamishwa,
Wala malalamiko katika njia zetu.
15 #
Kum 33:29
Heri watu wenye hali hiyo,
Heri watu wenye BWANA kuwa Mungu wao.
Currently Selected:
Zaburi 144: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

:
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.