YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 145

145
Ukuu na wema wa Mungu
Sifa. Ya Daudi.
1Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza,
Nitalihimidi jina lako milele na milele.
2Kila siku nitakuhimidi,
Nitalisifu jina lako milele na milele.
3BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana,
Wala ukuu wake hauchunguziki.
4Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako,
Kitayatangaza matendo yako makuu.
5Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako,
Na matendo yako yote ya ajabu.
6Watu watayataja matendo yako ya kutisha,
Nami nitausimulia ukuu wako.
7Watasimulia juu ya ukuu wa wema wako mwingi.
Na wataiimba haki yako kwa sauti.
8 # Kut 34:6; Hes 14:18; Zab 86:5,15; 57:10; Omb 3:22,23; Yn 1:17 BWANA ni mwenye fadhili na huruma,
Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
9 # Zab 100:5; Nah 1:7; Mt 5:45; Mdo 14:17 BWANA ni mwema kwa watu wote,
Na rehema zake ziko juu ya vyote alivyoumba.#145:9 au kazi zake zote.
10 # Zab 19:1 Ee BWANA, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
11Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kusena uweza wako.
12Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
13Ufalme wako ni ufalme wa milele,
BWANA ni mwaminifu katika maneno yake yote,
Na mwenye fadhili katika matendo yake yote#145:13 Mistari hii miwili haiko katika makala ya Kiebrania, lakini iko katika makala ya Kigiriki iitwayo Septuaginta.
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
14BWANA huwategemeza wote waangukao,
Huwainua wote walioinama chini.
15Macho ya watu wote yakuelekea Wewe,
Nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16Waufumbua mkono wako,
Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.
17BWANA ni mwenye haki katika njia zake zote,
Na mwenye huruma katika matendo yake yote.
18 # Zab 91:1; Isa 61:10; Yn 14:23; Yak 4:8; 1 Yoh 2:24; Yud 1:23; Ufu 3:20; Yn 4:24 BWANA yuko karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa uaminifu.
19 # 1 Yoh 5:14 Hutimiza matakwa ya wote wamchao,
Na pia husikia kilio chao, na huwaokoa.
20 # 1 Pet 1:5 BWANA huwahifadhi wote wampendao,
Na wote wasio haki atawaangamiza.
21Kinywa changu kitazinena sifa za BWANA;
Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu
milele na milele.

Currently Selected:

Zaburi 145: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in