YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 148

148
Sifa kwa utukufu mkuu wa Mungu
1Haleluya.
Msifuni BWANA kutoka mbinguni;
Msifuni katika mahali palipo juu.
2 # Dan 7:10; Ebr 1:7 Msifuni, enyi malaika wake wote;
Msifuni, majeshi yake yote.
3Msifuni, jua na mwezi;
Msifuni, nyota zote zenye mwanga.
4 # 1 Fal 8:27 Msifuni, enyi mbingu za mbingu,
Nanyi maji mlioko juu ya mbingu.
5 # Ebr 11:3 Na vilisifu jina la BWANA,
Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.
6 # Yer 33:25 Amevithibitisha hata milele na milele,
Ametoa amri wala haitapita.
7 # Isa 43:20 Msifuni BWANA kutoka nchi,
Enyi nyangumi na vilindi vyote.
8Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke,
Upepo wa dhoruba utimizao neno lake.
9 # Isa 49:13 Milima na vilima vyote,
Miti yenye matunda na mierezi yote.
10Hayawani, na wanyama wafugwao,
Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa.
11 # Mdo 17:28 Wafalme wa dunia, na watu wote,
Wakuu, na watawala wote wa dunia.
12Vijana wa kiume, na wanawali,
Wazee, na watoto;
13 # Isa 6:3; Flp 2:9 Na walisifu jina la BWANA,
Maana jina lake peke yake limetukuka;
Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.
14 # Efe 2:17; 1 Pet 2:9 Naye amewainulia watu wake pembe,
Sifa za watauwa wake wote;
Wana wa Israeli, watu walio karibu naye.
Haleluya.

Currently Selected:

Zaburi 148: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Zaburi 148