YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 60

60
Sala ya ushindi wa kitaifa baada ya kushindwa
Kwa mwimbishaji: kwa kufuata mtindo wa Shushani Eduthi. Utenzi wa Daudi; wa kufundisha; wakati alipopambana na Waaramu. Kutoka Naharaimu na Zoba, na Yoabu alipowaua Waedomi 12,000 katika Bonde la Chumvi alipokuwa akirudi.
1Ee Mungu, umetutupa na kututawanya,
Umekuwa na hasira, uturudishe tena.
2Umeitetemesha nchi na kuipasua,
Upaponye palipobomoka, maana inatikisika.
3Umewaonesha watu wako mazito,
Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.
4 # Isa 11:10 Umewapa wakuogopao bendera,
Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.
5 # Zab 108:6 Ili wapenzi wako waopolewe,
Utuokoe kwa mkono wako wa kulia, utuitikie.
6 # Zab 89:35; Mwa 12:6; Yos 13:27 Mungu amenena kwa utakatifu wake,
Nami nikishangilia.
Nitaigawanya Shekemu,
Na kulipima bonde la Sukothi.
7 # Kum 33:17; Mwa 49:10 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu,
Na Efraimu ni kinga ya kichwa changu.
Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,
8Moabu ni bakuli langu la kunawia.
Nitamtupia Edomu kiatu changu,
Na kumpigia Filisti kelele za vita.
9Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye boma?
Ni nani atakayeniongoza hadi Edomu?
10 # Zab 44:9 Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa?
Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?
11Utuletee msaada juu ya mtesi,
Maana wokovu wa binadamu haufai kitu.
12 # 1 Nya 19:13 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,
Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.

Currently Selected:

Zaburi 60: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Zaburi 60