YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 62

62
Wimbo wa kusifia imani kwa Mungu pekee
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.
1Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa utulivu,
Wokovu wangu hutoka kwake.
2Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,
Ngome yangu, sitatikisika.
3 # Isa 30:13 Hadi lini mtamshambulia mtu,
Mpate kumwua ninyi nyote pamoja?
Kama ukuta unaoinama,
Kama ua ulio tayari kuanguka,
4 # Zab 28:3 Mpango wao ni kumwangusha tu mtu mwenye cheo;
Huufurahia uongo.
Kwa kinywa chao hubariki;
Kwa moyo wao hulaani.
5 # Mik 7:7,10 Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa utulivu.
Maana tumaini langu hutoka kwake.
6Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,
Ngome yangu, sitatikisika.
7 # Yer 3:23 Kwa Mungu wokovu wangu,
Na utukufu wangu;
Mwamba wa nguvu zangu,
Na kimbilio langu ni kwa Mungu.
8 # 1 Sam 1:15; Zab 42:4 Enyi watu, mtumainini sikuzote,
Ifunueni mioyo yenu mbele zake;
Mungu ndiye kimbilio letu.
9Hakika binadamu ni ubatili,
Na wenye cheo ni uongo,
Katika mizani huinuka;
Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
10 # Isa 26:4; Mk 10:23; Lk 12:15 Msiitumainie dhuluma,
Wala msijivune kwa unyang'anyi;
Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
11Mara moja amenena Mungu;
Mara mbili nimeyasikia haya,
Ya kuwa nguvu zina Mungu,
12 # Ayu 34:11; Yer 17:10; Mt 16:27; 1 Pet 1:17; Rum 2:6; Ufu 2:23 Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana;
Maana ndiwe umlipaye kila mtu
Kulingana na haki yake.

Currently Selected:

Zaburi 62: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Zaburi 62