YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 64

64
Sala ya ulinzi kutoka kwa adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu;
Unilinde uhai wangu kutoka kwa hofu ya adui.
2 # Zab 143:9 Unifiche mbali na njama za watenda mabaya,
Mbali na mipango ya watu wafanyao maovu;
3 # Zab 57:4 Waliounoa ulimi wao kama upanga,
Wanaoyalenga maneno ya uchungu kama mishale,
4Wapate kumpiga mkamilifu faraghani,
Kwa ghafla humpiga bila kuogopa.
5Walijifanya hodari katika jambo baya;
Hushauriana juu ya kutega mitego;
Wakisema, Ni nani atakayeiona?
6Ni nani atambuaye maovu yetu?
Tumepanga njama kwa werevu mwingi,
Maana katika moyo wa mtu na fikira mengi yamefichika.#64:6 Maana ya mstari huu si dhahiri kwa Kiebrania.
7Lakini Mungu atawapiga kwa mshale wake,
Na kuwajeruhi ghafla.
8 # Mit 12:13 Kwa ajili ya ulimi wao wataangamizwa;
Wote wawaonao watatetemeka kwa hofu.
Wote wawaonao watatikisa kichwa.
9Na watu wote wataogopa,
Wataitangaza kazi ya Mungu,
Na kuyafahamu matendo yake.
10 # Zab 32:11; Flp 4:4 Mwenye haki atamfurahia BWANA na kumkimbilia,
Na wote wenye moyo wa adili watasifu.

Currently Selected:

Zaburi 64: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Zaburi 64