YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 74

74
Ombi la kutaka msaada wakati wa kushindwa
Utenzi wa Asafu.
1 # Zab 95:7; Yer 23:1; Eze 34:8,31; Lk 12:32 Ee Mungu, mbona umetutupa milele?
Kwa nini hasira yako inatoka moshi
Juu ya kondoo wa malisho yako?
2Ulikumbuke kusanyiko lako,
Ulilolinunua zamani.
Ulilolikomboa liwe kabila la urithi wako,
Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako.
3Upite na kupaona palipoharibika milele;
Adui ameufanya kila ubaya katika patakatifu.
4 # Dan 6:27 Watesi wako wamenguruma kati ya kusanyiko lako;
Wameweka bendera zao ziwe alama.
5Wanaonekana kama watu wainuao mashoka,
Waikate miti ya msituni.
6Na sasa nakishi yake yote pia
Wanaivunjavunja kwa mashoka na nyundo.
7Wamepatia moto patakatifu pako;
Wamelinajisi kao la jina lako hata chini.
8 # Zab 83:4 Walisema mioyoni mwao,
Na tuwaangamize kabisa;
Mahali penye mikutano ya Mungu
Wamepachoma moto katika nchi pia.
9 # 1 Sam 3:1; Mik 3:6; Mt 16:4 Hatuzioni ishara zetu, wala sasa hakuna nabii,
Wala kwetu hakuna ajuaye, hadi lini?
10Ee Mungu, mtesi atalaumu hata lini?
Adui alidharau jina lako hata milele?
11Mbona unaurudisha mkono wako,
Naam, mkono wako wa kulia,
Uutoe kifuani mwako,
Ukawaangamize kabisa.
12 # Zab 44:4 Lakini Mungu ni mfalme wangu tokea zamani,
Afanyaye mambo ya wokovu katikati ya nchi.
13 # Kut 14:21; Isa 51:9 Wewe umeipasua bahari kwa nguvu zako,
Umevivunja vichwa vya nyangumi juu ya maji.
14 # Kut 17:5,6; Hes 14:9; Hes 20:11; Ayu 41:1; Isa 11:16; Isa 27:1; Yos 3:13; Zab 72:9; Zab 104:26; Zab 105:41; Hab 3:9; Ufu 16:12 Wewe ulivivunja vichwa vya Lewiathani,
Awe chakula cha watu wa jangwani.
15Wewe ulitokeza chemchemi na kijito;
Wewe ulikausha mito yenye maji sikuzote.
16Mchana ni wako, usiku nao ni wako,
Ndiwe uliyeufanya mwanga na jua.
17 # Mdo 17:26 Wewe uliiweka mipaka yote ya dunia,
Majira ya joto na ya baridi wewe uliyafanya.
18 # Ufu 16:19 Ee BWANA, uyakumbuke hayo, adui amelaumu,
Na watu wapumbavu wamelidharau jina lako.
19 # Wim 2:14; 4:1 Usimpe mnyama mkali uhai wa njiwa wako;
Usiwasahau milele watu wako walioonewa.
20 # Mwa 17:7; Law 26:44; Yer 33:21 Ulitafakari agano lako;
Maana mahali kwenye giza katika nchi
Kumejaa makao ya ukatili.
21 # Zab 9:18 Aliyeonewa asirejee ametiwa haya,
Mnyonge na mhitaji na walisifu jina lako.
22 # Isa 37:23 Ee Mungu, usimame, ujitetee mwenyewe,
Ukumbuke unavyotukanwa na mpumbavu mchana kutwa.
23Usiisahau sauti ya watesi wako,
Ghasia yao wanaokupinga inapaa daima.

Currently Selected:

Zaburi 74: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

Videos for Zaburi 74