YouVersion Logo
Search Icon

Ufunuo 10

10
Malaika aliye na kitabu kidogo
1 # Ufu 4:3; 5:2 Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto. 2Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kulia juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi. 3#Yer 25:30; Hos 11:10; Amo 1:2 Naye akaita kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao. 4#Dan 8:26; 12:4,9 Na ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nilikuwa tayari kuandika. Nami nilisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie mhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo ngurumo saba, usiyaandike. 5#Kut 20:11; Kum 32:40; Dan 12:7; Amo 3:7 Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kulia kuelekea mbinguni, 6#Mwa 14:19,22; Neh 9:6; Kut 20:11; Zab 146:6; Ufu 6:11; Dan 12:7 akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na kukawia tena baada ya haya; 7#Amo 3:7; Dan 9:6,10; Zek 1:6; Mdo 3:21; Ufu 11:15; 17:17 isipokuwa katika siku za sauti ya malaika wa saba atakapokuwa tayari kupiga baragumu; hapo ndipo siri ya Mungu itakapotimizwa, kama alivyowatangazia watumishi wake hao manabii. 8#Eze 2:8—3:3 Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Nenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi. 9#Eze 2:8; 3:1-3 Nikamwendea malaika yule nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho kitakutia uchungu tumboni mwako, bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama asali. 10Nikakitwaa kile kitabu kidogo kutoka mkononi mwa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu. 11#Yer 1:10; 25:30; Dan 3:4; 7:14 Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi.

Currently Selected:

Ufunuo 10: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in