YouVersion Logo
Search Icon

Ruthu UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu hiki kimepewa jina la mwanamke ambaye habari zake ndizo simulizi kuu, yaani Ruthu, Mmoabi.
Elimeleki, mkewe Naomi na watoto wao wa kiume, Maloni na Kilioni wa kabila la Efraimu walitoka Yuda wakaenda kuhemea katika nchi ya Moabu. Kwa kuwa walikaa huko kwa muda watoto wao walioa Wamoabi, Orpa na Ruthu. Baadaye Elimeleki na wanawe wawili wakafariki. Orpa, Ruthu na mama mkwe wao Naomi wote wakawa wajane. Naomi aliamua kurudi nyumbani Bethlehemu. Ruthu aliambatana na Naomi hadi Yuda. Kisha Ruthu akaolewa na Boazi, mtu mwenye sifa ya bidii, roho nzuri, tajiri na aliyekuwa jamaa ya mumewe marehemu.
Masimulizi ya Kitabu hiki yanavutia sana. Uhusiano kati ya mwanamke na wakwe zake, mwajiri na wafanya kazi na maofisa wa mji na raia unatuonesha muundo wa utaratibu wa maisha yenye upendo, maisha ya kumtii Mungu na kumpenda jirani kama nafsi yake. Kilele cha masimulizi juu ya Ruthu ni aliyedhaniwa kuwa amepoteza kila kitu anaingia kwenye chimbuko la Mfalme Mkuu kuliko wote katika historia ya Israeli yaani Mfalme Daudi na Yesu Kristo.
Yaliyomo:
1. Utangulizi, Sura 1:1-5
2. Naomi na wakwe zake Wamoabi, Sura 1:6-22
3. Maisha mapya katika Yuda, Sura 2:1—4:12
4. Masimulizi juu ya nasaba ya Daudi, Sura 4:13-22

Currently Selected:

Ruthu UTANGULIZI: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in