YouVersion Logo
Search Icon

Tito UTANGULIZI

UTANGULIZI
Tito hatajwi katika safari za Paulo za kitume zilizoandikwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume. Lakini katika Gal 2:1-3 tunajua kwamba Tito aliandamana na Paulo alipotembelea Yerusalemu wakati ambapo Paulo alitambuliwa kuwa mtume na viongozi wa kule Yerusalemu. Tunajua pia kwamba alikuwa Mgiriki na hivyo basi hakutahiriwa, jambo ambalo lilizusha ubishi mkubwa huku wengi wakimtaka atahiriwe. Hata hivyo Paulo alipinga sana jambo hilo.
Paulo alimwona Tito kuwa mwaminifu akamtumia mara mbili kule Korintho ambako alifaulu kuweka tena uhusiano mwema kati ya Paulo na kanisa la Korintho (2 Kor 7:6-7). Alimtuma pia kwa makanisa mengine mbalimbali ili atatue matatizo yaliyokuwepo ili kuyasimamia na kumpelekea Paulo taarifa za maendeleo ya makanisa machanga (2 Kor 2:3-4,9,12-13; 7:5-8, 13-15; 8:1-6,16-24; 12:18).
Mafundisho ya Waraka huu yanafanana na yale ya 1 Timotheo: Mambo yanayotakiwa kwa viongozi wa kanisa – “maaskofu” na “wazee” (sura 1) wanapokabiliwa na mafundisho ya uongo; na sura ya 2 (2:1-10) namna ya kuwatendea watu wa vikundi mbalimbali vya jumuiya ya Kikristo (2:1-10). Mafundisho juu ya kuhesabiwa haki na wokovu kwa njia ya neema ya Mungu, na juu ya kazi ya Roho Mtakatifu (2:11,14 na 3:4-7) ni msingi wa maneno ya Paulo ya kuhimiza na kutia moyo kwamba inampasa Tito awe imara katika kuongoza na kulipa kanisa mafundisho ya kiroho (3:1-3,8-11).

Currently Selected:

Tito UTANGULIZI: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in