Yohana MT. 17
17
1MANENO hayo aliyasema Yesu: akainua macho yake kuelekea mbinguni, akanena, Baba, saa ile imekuja. Mtukuze Mwana wako, illi Mwana wako nae akutukuze wewe; 2kama vile ulivyompa mamlaka juu ya killa mwenye mwili, illi yote uliyompa awape uzima wa milele. 3Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. 4Mimi nimekutukuza duniani. Kazi ile uliyonipa niifanye nimeimaliza. 5Na sasa unitukuze wewe, Baba, pamoja nawe, kwa utukufu nle niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya kuwako ulimwengu. 6Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; wahkuwa wako, ukanipa mimi: na neno lako wamelishika. 7Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako: 8kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma. 9Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu, bali wao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako. 10Na yote yaliyo yangu ni yako, na yaliyo yako ni yangu: nami nimetukuzwa ndani yao. 11Na mimi simo tena ulimwenguni, na hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, uwalinde kwa jina lako wale ulionipa; wawe moja, kama sisi. 12Nilipokuwa pamoja nao ulimwenguni, mimi naliwalinda kwa jina lako: wale ulionipa naliwatunza, wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, illa yule mwana wa upotevu maandiko yapate kutimizwa. 13Na sasa naja kwako; na haya nayasema ulimwenguni, illi wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. 14Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu uliwachukia, kwa kuwa wao si watu wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 15Siombi uwatoe katika ulimwengu, hali uwalinde na yule mwovu. 16Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisiyvo wa ulimwengu. 17Uwatakase kwa kweli; neno lako ndio kweli. 18Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma wao ulimwenguni. 19Na kwa ajili yao najitakasa, illi na hawa watakaswe katika kweli. 20Wala si hao tu ninaowaombea, bali na wao walakaoniammi kwa sababu ya neno lao. 21Wote wawe umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako, illi na hawa wawe umoja ndani yetu: ulimwengu upate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma. 22Nami, utukufu ule ulionipa nimewajia wao, wawe umoja, kama sisi tulivyo umoja: 23mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, wapate kukamilika na kuwa umoja; illi ulimwengu ujue ya kuwa udiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. 24Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. 25Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nalikujua; na hawa walijua ya kuwa ndiwe uliyenituma. 26Naliwajulisiia jina lako, tena nitawajulisha, illi pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, na mimi niwe ndani yao.
Currently Selected:
Yohana MT. 17: SWZZB1921
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.