Mattayo MT. 20
20
1KWA maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. 2Na alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, akawapeleka katika shamba lake la mizabibu. 3Akatoka muamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; 4na hawo nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo liaki nitakupeni. Wakaenda. 5Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vilevile. 6Hatta mnamo saa edashara akatoka, akakuta wengine wakisimama wasiokuwa na kazi, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi? 7Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, Enendeni na ninyi katika shamba la mizabibu, na iliyo haki mtapata. 8Kulipokuchwa, yule bwana wa mizabibu akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ijara yao, ukianzia wa mwisho hatta wa kwanza. 9Walipokuja wale wa saa edashara, wakapokea killa mtu dinari. 10Na wale wa kwanza walipokuja, wakadhani watapokea zaidi; na wao pia wakapokea killa mtu dinari. 11Wakiisha kupokea, wakamnungʼunikia mwenye nyumba, 12wakinena, Hawa wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana. 13Nae akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari? 14Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe. 15Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu nipendavyo? Au jicho lako ni ovn kwa sababu ya kuwa mimi mwema? 16Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza wa mwisho: maana waitwao wengi, hali wateule wachache.
17Hatta Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemi, aliwachukua wanafunzi thenashara kwa faragha njiani, akawaambia, 18Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemi; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa makuhani wakuu na waandishi; nao watamhukumu afe; 19na watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulibi; na siku ya tatu atafufuka.
20Ndipo mama ya wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akimsujudia, akimwomba neno. 21Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza hawa wanangu waketi mmoja mkono wako wa kunme; na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako. 22Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomha. Mwaweza kuuywea kikombe nitakachonywea mimi, na kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi? Wakamwambia, Twaweza. 23Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu, na mtabatizwa ubatizo nibatizwao mimi; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri niwapeni, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.
24Na wale kumi waliposikia, wakawakasirikia wale ndugu wawili. 25Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wafalme wa Mataifa huwatawala, na wakuu wao huwatumikisha. 26Lakini kwemi ninyi haitakuwa hivi: bali ye yote atakae kuwa mkuu kwenu, na awe mkhudumu wenu; 27na ye yote atakae kuwa wa kwanza kwenu awe mtumishi wenu: 28kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kukhudumiwa, bali kukhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.
29Hatta walipokuwa wakitoka Yeriko mkutano mkubwa wakamfuata. 30Na vipofu wawili wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba Yesu anapita, wakapaaza sauti zao, wakinena, Uturehemu, Ee Bwana, mwana wa Daud! 31Makutano wakawakaripia, wanyamaze. Lakini wao wakazidi kupaaza sauti zao, wakinena, Uturehemu, Ee Bwana, mwana wa Daud! 32Yesu akasimama, akawaita, akasema, Mnataka niwafanyie nini? 33Wakamwambia, Bwana, macho yetu yafumbuliwe. 34Yesu akawahurumia, akawagusa macho yao; marra macho yao yakapata kuona, wakamfuata.
Currently Selected:
Mattayo MT. 20: SWZZB1921
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.