Marko MT. 5
5
1WAKAFIKA ngʼambu ya bahari hatta inchi ya Wageraseni. 2Na alipokwisha kushuka chomboni, marra akakutwa na mtu ambae ametoka makaburini, nae ana pepo mchafu, makao yake yalikuwa pale makaburini: 3wala hakuna mtu aliyeweza kumfunga, hatta kwa minyororo: 4kwa sababu alikuwa amefungwa marra nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunjavunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. 5Na siku zote, usiku na mchana, alikuwa makaburini na milimani, akilia na kujikata kwa mawe. 6Alipomwona Yesu kwa mbali, akampiga mbio, akamsujudia; 7akalia kwa sauti kuu akanena, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi, uniapie kwa Mungu kwamba hutaniadhibu. 8Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. 9Akamwambia, Jina lako nani? Akajibu, akamwambia, Jina langu Legioni: kwa kuwa tu wengi. 10Akamsihi sana asiwapeleke nje ya incbi ile. 11Na pale milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, walisha. 12Pepo wote wakamsihi, wakinena, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. 13Akawapa rukhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale ngumwe: kundi lote likatelemka kwa kassi gengeni, wakaingia baharini; walikuwa wapata elfeen; wakafa baharini. 14Wachungaji wa wale nguruwe wakakimbia wakaeneza khahari mjini na mashamba. Wakatoka waone khabari iliyotukia. 15Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, nae ndiye aliyekuwa na ile legione; wakaogopa. 16Nao walioona wakaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na khabari za nguruwe. 17Wakaanza kumsihi atoke katika mipaka yao. 18Alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi awe pamoja nae: 19Yesu hakumrukhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawakhubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. 20Akaenda zake, akaanza kukhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakataajabu.
21Hatta Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ngʼambu katika kile chombo, wakamkusanyikia makutano mengi: nae alikuwa kando ya bahari. 22Kumbe! akaja mtu mmoja katika wakuu wa sunagogi, jina lake Yairo: hatta alipomwona, akaanguka miguuni pake, 23akimsihi sana, akinena. Binti yangu mdogo yu katika kufa: nakuomba nje, nweke mkono wako juu yake, apate kupona, nae ataishi. 24Akaenda pamoja nae: makutano mengi wakamfuata, wakimsongasonga. 25Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka thenashara, 26na kuteswa mengi kwa mikono ya tabibu wengi, akagharimu vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hatta kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya, 27bassi aliposikia khabari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; 28maana alinena, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. 29Marra chemchemi ya damu yake ikakauka, akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. 30Marra Yesu akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya makutano, akanena, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? 31Wanafunzi wake wakamwambia, Wawaona makutano wanavyokusongasonga, nawe wanena, Ni nani aliyenigusa? 32Akatazama pande zote illi amwone yule aliyelitenda neno hili. 33Na yule mwanamke akaingiwa na khofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. 34Akamwambia, Binti imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, ukawe mzima, usiwe na msiba wako tena. 35Hatta alipokuwa akisema wakaja watu kutoka kwa mkuu wa sunagogi, wakinena, Binti yako amekwisha kufa: ya nini kuzidi kumsumbua mwalimu? 36Yesu, marra alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sunagogi, Usiogope, amini tu. 37Wala hakumrukhusu mtu afuatane nae, illa Petro, na Yakobo, na Yohana ndugu yake Yakobo. 38Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sunagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo mengi. 39Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hakufa, bali amelala tu. Wakamcheka sana. 40Nae alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa baba yake yule mtoto na mama yake, na wale walio pamoja nae, akaingia ndani alimokuwamo yule mtoto. 41Akamshika mkono yule kijana, akamwambla, Talitha, kumi: tafsiri yake, Kijana, nakuambia, Ondoka. 42Marra akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata miaka thenashara. Wakashangaa mshangao mwingi. 43Akawaagiza sana, mtu asijue khabari ile; akaamuru apewe chakula.
Currently Selected:
Marko MT. 5: SWZZB1921
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.