2 Mose 12
12
Kondoo ya Pasaka.
(1-28: 2 Mose 23:15; 34:18; 3 Mose 23:5-14; 4 Mose 9:1-14; 28:16-25; 5 Mose 16:1-8; 1 Kor. 5:7)
1Bwana akamwambia Mose na Haroni katika nchi ya Misri kwamba: 2Mezi huu sharti uwawie wa kwanza a miezi, uwe wenu wa kwanza wa kuihesabu miezi ya mwaka.#1 Mose 13:4. 3Uambieni mkutano wote wa wana wa Isiraeli kwamba: Siku ya kumi ya mwezi huu kila mwenye nyumba na achukue mwana kondoo, watu wa kila nyumba moja mwana kondoo mmoja! 4Lakini kama watu wa nyumba moja ni wachache, wsiweze kumaliza mwana kondoo, basi, yeye na jirani yake wa kukaa karibu ya nyumba yake watachukua mmoja kwa hesabu yao waliomo humo nyumbani; kwa hivyo, watu wanavyoweza kula, na mmhesabie mwana kondoo watu wa kumla. 5Nanyi na mchukue mwana kondoo asiye na kilema, aliye wa kiume mwenye mwaka mmoja, akiwa mwana kondoo au mwana mbuzi.#3 Mose 22:20. 6Na mwe naye na kumwangalia mpaka siku ya kumi na nne ya mwezi huu; ndipo watu wote pia wa mkutano wa Waisiraeli wamchinje saa za jioni. 7Nayo damu yake ya kutosha na wachukue ya kuipaka miimo yote miwili ya mlango na kizingiti cha juu katika hizo nyumba, watakamolia.#2 Mose 12:13,22. 8Usiku uleule na wazile nyama zake, nazo ziwe zimechomwa motoni. Na wazile pamoja na mikate isiyochachwa na pamoja na mboga chungu. 9Msizile, zikiwa mbichi, wala zikiwa zimepikwa majini, ila sharti ziwe zimechomwa nzima motoni, kichwa kikiwa pamoja na paja zake na utumbo wake. 10Wala mzisaze nyama nyingine hata asubuhi! Ila zitakazosalia hata asubuhi mziteketeze kwa moto! 11Tena hivi ndivyo, mtakavyozila: Viuno vyenu na viwe vimefungwa, namo miguuni mwe mmevaa viatu, nazo fimbo zenu na mzishike mikononi mwenu. Hivyo mzile kama watu wanaojihimiza kwenda safari. Kwani hii ndio Pasaka ya Bwana.#Yes. 52:12. 12Nami nitapita usiku uleule katika nchi yote ya Misri, nimpige kila mwana wa kwanza katika nchi ya Misri aliye wa wwatu pamoja nao walio wa nyama wa kufuga, nayo miungu yote ya Misri nitaihukumu mimi Bwana.#4 Mose 33:4. 13Nazo zile damu penye nyumba mlimo zitakuwa kielekezo chenu: nitakapoziona nitapita kwenu, lisiwapate ninyi lile pigo la mwangamizaji, nitakapoipiga nchi ya Misri.#Ebr. 11:28.
14Siku hiyo sharti iwe kwenu ya kuikumbuka, mwilie sikukuu ya Bwana. Haya na yawe maongozi ya kale na kale kwa vizazi vyenu vijvyo, mwilie sikukuu. 15Siku saba na mle mikate isiyochachwa. Siku ya kwanza sharti mkomeshe chachu na kuziondoa nyumbani mwenu, kwani kila atakayekula siku ya kwanza mpaka siku ya saba yaliyo yenye chachu sharti huyo ang'olewe kwao Waisiraeli.#2 Mose 13:7. 16Siku ya kwanza sharti mkutanie Patakatifu, nayo siku ya saba mkutanie Patakatifu; siku hizo zisifanywe kazi zo zote, kazi iliyo na ruhusa kwenu peke yake tu ni hiyo ya chakula cha kila mtu. 17Iangalieni hiyo mikate isiyochachwa! Kwani siku hiyo ndipo papo hapo, nilipovitoa vikosi vyenu katika nchi ya Misri. Kwa hiyo iangalieni siku hiyo! Haya na yawe maongozi ya kale na kale kwa vizazi vyenu vijavyo. 18Siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza jioni na mle mikate isiyochachwa mpaka jioni ya siku ya ishirini na moja ya mwezi huo. 19Siku saba chachu isionekane nyumbani mwenu, kwani kila atakayekula iliyo yenye chache siku hizo sharti huyo ang'olewe katika mkutano wa Waisiraeli, kama ni mgeni, au kama ni mzalia wa nchi hiyo. 20Msile cho chote chenye chachu siku hizo, ila po pote, mtakapokaa, sharti mle mikate isiyochachwa.
21Mose akawaita wazee wote wa Waisiraeli, akawaambia: Haya! Nendeni, mchukue wana kondoo wa kuwatoshea ndugu wa nyumbani mwenu, mwachinje kuwa wa Pasaka! 22Tena chukueni vitita vya vivumbasi, mvichovye katika damu iliyotiwa katika bakuli, mkinyunyizie kizingiti cha juu na miimo yote miwili ya mlango hiyo damu iliyotiwa katika bakuli, tena mtu ye yote wa kwenu asitoke mlangoni mwa nyumbani mwake, mpaka kuche. 23Naye Bwana atapita kuwapiga wana wa kwanza wa Misri; hapo, atakapoona damu penye kizingiti cha juu na penye miimo yote miwili, basi, Bwana ataupita mlango huo, asimpe mwangamizaji ruhusa kuingia nyumbani mwenu na kuwapiga. 24Nalo neno hili sharti mliangalie kuwa maongozi yako na ya wanao kale na kale. 25Napo hapo, mtakapoingia katika hiyo nchi, Bwana atakayowapa, kama alivyosema, sharti mwuangalie utumishi huu. 26Tena hapo, wana wenu watakapowauliza: Huu utumishi wenu maana yake nini?#1 Mose 18:19; 5 Mose 6:7,20. 27na mwaambie: Hii ndio ng'ombe ya tambiko ya Pasaka ya Bwana, kwa kuwa alizipita nyumba za wana wa Isiraeli huko Misri, akaziponya nyumba zetu alipowapiga Wamisri. Ndipo, watu walipoinama na kumwangukia Mungu. 28Kisha wana wa Isiraeli wakaenda, wakafanya, kama Bwana alivyomwagiza Mose na Haroni; hivyo ndivyo, walivyofanya.
Pigo la kumi: Wana wa kwanza wa Misri wanauawa.
29Ulipokuwa usiku wa manane, Bwana akawapiga wana wa kwanza wote katika nchi ya Misri, kuanzia mwana wa kwanza wa Farao aliyekaa katika kiti chache cha kifalme, kuishia mwana wa kwanza wa mfungwa aliyekuwa chumbani kifungoni nao wana wote wa kwanza wa nyama wa kufuga.#2 Mose 4:23. 30Ndipo, Farao alipoamka usiku, yeye na watumishi wake wote na Wamisri wote, maombolezo yakawa makuu huko Misri, kwani hakuna nyumba isiyokuwa na mfu. 31Naye akamwita Mose na Haroni usiku, akawaambia: Ondokeni, mtoke katikati yao walio ukoo wangu, ninyi na wana wa Isiraeli! Nendeni kumtumikia Bwana, kama mlivyosema! 32Nao mbuzi na kondoo na ng'ombe wenu wachukueni, kama mlivyosema! Haya! Nendeni, mnibariki nami!#2 Mose 10:26. 33Wamisri nao wakawahimiza hao watu na kuwatoa upesi katika nchi yao, kwani walisema: Sisi sote tutakufa.#2 Mose 6:1.
Waisiraeli wanaanza kutoka Misri.
34Watu wakauchukua unga wao uliokandwa, ukiwa haujachachuka bado, nayo mabakuli yao ya kukandia wakayafunga katika nguo zao, wakayachukua mabegani. 35Nao wana wa Isiraeli walikuwa wameyafanya, Mose aliyowaambia, wakiwatakia Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu na nguo.#2 Mose 11:2. 36Naye Bwana aliwapatia hawa watu upendeleo machoni pa Wamisri, nao wakawakopesha; hizi ndizo nyara, walizoziteka huko Misri.#2 Mose 3:21.
37Hivyo ndivyo, wana wa Isiraeli walivyoondoka Ramusesi kwenda Sukoti, nao walikuwa wanawaume tu waliokwenda kwa miguu 600000 pasipo watoto. 38Nao wengine wengi waliochanganyika nao wakapanda nao, tena mbuzi na kondoo na ng'ombe, kundi kubwa sana. 39Nao ule unga uliokandwa, waliouchukua walipotoka Misri, wakauoka kuwa maandazi na mikate isiyochachwa, kwani ulikuwa haukuchachuka, kwani walikimbizwa kutoka Misri, hawakuweza kukawilia wala kutengeneza pamba za njiani.
40Miaka ya kukaa, wana wa Isiraeli waliyokaa Misri, ilikuwa miaka 430.#1 Mose 15:13. 41Hii miaka 430 ilipokwisha pita, siku iyo hiyo vikosi vyote vya Bwana vilitoka katika nchi ya Misri. 42Usiku huo wa kuwatoa katika nchi ya Misri ulikuwa usiku wa Bwana wa kuangaliwa; kwa hiyo usiku huo wa Bwana na uwe wa kuangaliwa kwa wana wote wa Isiraeli na kwa vizazi vyao vijavyo.
Maongozi ya sikukuu ya Pasaka.
43Bwana akamwambia Mose na Haroni: Haya ndiyo maongozi ya Pasaka: mtu asiye wa kwenu asiile! 44Lakini kila mtumwa aliyenunuliwa kwa fedha ataila, ukiisha kumtahiri. 45Atakayekaa tu kwako na mtu wa mshahara asiile! 46Sharti iliwe katika kila nyumba, lakini usitoe nyama yake yo yote mle nyumbani na kuipeleka nje, wala msimvunje mfupa wo wote!#Yoh. 19:36. 47Wao wote wa mkutano wa Waisiraeli sharti wafanye hivyo. 48kama mgeni anakaa ugenini kwako, naye akitaka kuila Pasaka ya Bwana, uwatahiri wote walio wa kiume kwake, kisha ataweza kuikaribia kuila, maana atakua kama mzalia wa hiyo nchi, lakini kila asiyetahiriwa asiile! 49Maonyo yawe yayo hayo ya mzalia wa kwenu nayo ya mgeni atakayekaa ugenini kwako!#3 Mose 24:22. 50Nao wana wa Isiraeli wote wakayafanya; kama Bwana alivyomwagiza Mose na Haroni, ndivyo, walivyofanya.
51Ilikuwa siku ileile moja tu, Bwana akiwatoa wana wa Isiraeli katika nchi ya Misri vikosi kwa vikosi.
Currently Selected:
2 Mose 12: SRB37
Highlight
Share
Copy

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.