Yohana 15
15
Mzabibu na matawi yake.
1*Mimi ni mzabibu wa kweli naye Baba yangu ndiye mpalilizi. 2Kila tawi langu lisilozaa huliondoa; lakini kila tawi lizaalo hulitakasa akilipogoa, lipate kuzaa mengi. 3Ninyi mmekwisha kutakata mkilipokea lile Neno, nililowaambia. 4Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu! Kama tawi lisivyoweza kuzaa likiwa peke yake, lisipokaa mzabibuni, vivyo hivyo nanyi hamna mwezacho, msipokaa ndani yangu. 5Mimi ni mzabibu, ninyi m matawi. Anayekaa ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa mengi. Kwani pasipo mimi hamna mwezacho kukifanya.#2 Kor. 3:5. 6Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi, likikauka; kisha watu huyakusanya pamoja na kuyatupa motoni yateketee. 7Mtakapokaa ndani yangu, nayo maneno yangu yatakapokaa ndani yenu, mtaomba lo lote, mnalolitaka, kisha mtalipata.#Mar. 11:24. 8Hapo ndipo, Baba yangu anapotukuzwa, mnapozaa mengi, mkawa wanafunzi wangu.*#Mat. 5:16.
9*Kama Baba alivyonipenda, ndivyo, nami ninavyowapenda ninyi. Kaeni na kunipenda! 10Mtakapoyashika maneno yangu mtakaa na kunipenda, kama mimi nilivyoyashika maagizo ya Baba yangu, nikakaa na kumpenda yeye.#Yoh. 14:15.
Upendano.
11Nimewaambia haya, furaha yangu iwakalie, nanyi furaha yenu itimie yote.#Yoh. 16:24; 17:13. 12Hili ndilo agizo langu: Mpendane, kama nilivyowapenda!#Yoh. 13:34. 13Hakuna mwenye upendo kumpita mwenye kujitoa, awaokoe wapenzi wake.#Yoh. 10:12; 1 Yoh. 3:16. 14Ninyi m wapenzi wangu mkiyafanya, ninayowaagiza.#Yoh. 8:31; Mat. 12:50. 15Sitawaita tena watumwa, kwani mtumwa hayajui, bwana wake anayoyafanya. Nimewaita wapenzi, kwani yote, niliyoyasikia kwa Baba yangu, nimewatambulisha ninyi. 16Sio ninyi mlionichagua, lakini ndiye mimi niliyewachagua ninyi, nikawaweka, mwende kuzaa matunda, nayo matunda yenu yakae; kwa hiyo Baba atawapa lo lote, mtakalomwomba katika Jina langu.* 17Haya nawaagizani: Mpendane!
Kuchukiwa na ulimwengu.
18Ulimwengu ukiwachukia, tambueni, ya kuwa mimi ni mtangulizi wenu aliyeanza kuchukiwa nao!#Yoh. 7:7. 19Kama mngekuwa wa ulimwengu, wao wa ulimwengu wangewapenda, kwamba m wenzao. Lakini kwa sababu ham wa ulimwengu, kwani mimi naliwachagua na kuwatoa ulimwenguni, kwa hiyo wao wa ulimwengu huwachukia.#Yoh. 17:14; Luk. 6:22; 1 Yoh. 4:5. 20Likumbukeni lile neno, nililowaambia: Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake! Kama wamenifukuza mimi, watawafukuza nanyi.#Yoh. 13:16. 21Kama wamelishika Neno langu, hata lenu watalishika. Lakini hayo yote watawafanyia kwa ajili ya Jina langu, kwani hawamjui aliyenituma.#Yoh. 16:3. 22Kama singalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na kosa; lakini sasa hawana, watakalojikania makosa yao. 23Mwenye kunichukia mimi humchukia naye Baba yangu.#Yoh. 5:23; Luk. 10:16. 24Kama singalifanya kwao kazi, mwingine asizozifanya hata kale, wasingalikuwa na kosa. Lakini sasa wameziona, kisha wametuchukia, mimi na Baba yangu.#Yoh. 14:11. 25Lakini sharti litimie neno lililoandikwa katika Maonyo yao ya kwamba: Walinichukia bure.#Sh. 69:5.
26*Lakini atakapokuja mtuliza mioyo, nitakayemtuma toka kwa Baba, yule Roho wa kweli atakayetoka kwa Baba, ndiye atakayenishuhudia.#Yoh. 14:26; Luk. 24:49. 27Lakini nanyi m mashahidi, kwani tangu mwanzo mlikuwa pamoja nami.#Tume. 1:8,21-22; 5:32.
Currently Selected:
Yohana 15: SRB37
Highlight
Share
Copy
![None](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2F58%2Fhttps%3A%2F%2Fweb-assets.youversion.com%2Fapp-icons%2Fen.png&w=128&q=75)
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.