Hosea UTANGULIZI
UTANGULIZI
Hosea aliitwa kuwa msemaji wa Mungu katika nchi yake, yaani katika utawala wa kaskazini wa Israeli, mnamo mwaka 750-725 K.K. Alitanguliwa na nabii Amosi ambaye pia alihubiri katika utawala wa kaskazini wa Israeli.
Hosea anashutumu vikali ibada za miungu ya uongo ya nyakati zake na ukosefu wa imani kwa Mungu miongoni mwa Waisraeli. Hali hiyo ya kumwasi Mungu Hosea anailezea kwa picha ya maisha yake ya ndoa. Kama vile mkewe Gomeri alivyomgeuka na kuacha kuwa mwaminifu, ndivyo watu walivyomwacha Mungu. Kwa sababu hiyo, watu wa Israeli wataadhibiwa. Hata hivyo mwishowe Mungu, kwa upendo wake mkuu, atawarudisha na kurejesha uhusiano wake nao.
Sura 1–3 yaelezea maisha ya ndoa ya Hosea na mkewe ambayo ni kielelezo cha uasi wa Waisraeli kwa Mungu. Hosea anatangaza hukumu ya Mungu kwa watu wote, lakini anaonesha pia kwamba mwishowe upendo wa Mungu utashinda.
Sura 4–14 yahusu mahubiri mengine ya nabii.
Currently Selected:
Hosea UTANGULIZI: BHN
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.