Methali 9
9
Hekima na upumbavu
1Hekima amejenga nyumba yake,
nyumba yenye nguzo saba.
2Amechinja wanyama wa karamu,
divai yake ameitayarisha,
ametandika meza yake.
3Amewatuma watumishi wake wa kike mjini,
waite watu kutoka kwenye vilele vya miinuko:
4“Yeyote aliye mjinga na aje hapa!”
Na yeyote aliye mpumbavu humwambia:
5“Njoo ukale chakula,
na unywe divai niliyotengeneza.
6Achana na ujinga upate kuishi;
fuata njia ya akili.”
7Anayemkosoa mwenye dharau hupata matusi,
amkaripiaye mwovu huishia kwa kuumizwa.
8Usimwonye mwenye dharau maana atakuchukia;
mwonye mwenye hekima naye atakupenda.
9Mfunze mwenye hekima naye atazidi kuwa na hekima;
mfundishe mwadilifu naye atazidi kuelimika.
10 # Taz Yobu 28:28; Zab 111:10; Meth 1:7 Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa hekima;
na kumjua yule Mtakatifu ni kupata akili.
11Kwa msaada wangu mimi Hekima siku zako zitaongezwa;
utaongezewa miaka mingi maishani mwako.
12Kama una hekima, itakufaa wewe mwenyewe;
kama ukiidharau, mwenyewe utapata hasara.
13Mwanamke mpumbavu ana kelele,
hajui kitu wala hana haya.#9:13 aya 13 makala ya Kiebrania si dhahiri.
14Hukaa kitako mlangoni mwa nyumba yake,
huweka kiti chake mahali pa juu mjini,
15na kuwaita watu wapitao njiani,
watu wanaokwenda kwenye shughuli zao:
16“Yeyote aliye mjinga na aje hapa!”
Na yeyote aliye mpumbavu humwambia:
17“Maji ya wizi ni matamu sana;
mkate unaoliwa kwa siri ni mzuri sana.”
18Lakini mjinga hajui kwamba humo mna wafu,
wageni wa mwanamke huyo wamo chini Kuzimu.
Currently Selected:
Methali 9: BHN
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.