Zaburi 32
32
Maondoleo ya dhambi
(Zaburi ya Daudi. Funzo)
1 # Taz Rom 4:7-8 Heri yake mtu aliyesamehewa kosa lake,
mtu ambaye dhambi yake imeondolewa kabisa.
2Heri mtu ambaye Mwenyezi-Mungu hamwekei hatia,
mtu ambaye hana hila moyoni mwake.
3Wakati nilipokuwa sijakiri dhambi yangu,
nilikuwa nimedhoofika kwa kulia mchana kutwa.
4Mchana na usiku mkono wako ulinilemea;
nikafyonzwa nguvu zangu,
kama maji wakati wa kiangazi.
5Kisha nilikiri makosa yangu kwako;
wala sikuuficha uovu wangu.
Nilisema ninakuungamia makosa yangu ee Mwenyezi-Mungu,
ndipo nawe ukanisamehe dhambi zangu zote.
6Kwa hiyo, kila mwaminifu na akuletee maombi;
jeshi likaribiapo au mafuriko,
hayo hayatamfikia yeye.
7Wewe ndiwe kinga yangu;
wewe wanilinda katika taabu.
Umenijalia shangwe za kukombolewa.
8Mungu asema: “Nitakufunza
na kukuonesha njia unayopaswa kufuata.
Nitakushauri kwa uangalifu mkubwa.
9Usiwe mpumbavu kama farasi au nyumbu,
ambao lazima wafungwe lijamu na hatamu,
la sivyo hawatakukaribia.”
10Watu waovu watapata mateso mengi,
bali wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu wazungukwa na fadhili zake.
11Furahini na kushangilia kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu enyi waadilifu;
pigeni vigelegele vya shangwe enyi wanyofu wa moyo.
Currently Selected:
Zaburi 32: BHN
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.