Mwanzo 10
10
Wazawa wa Nuhu
1Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika. 2#1 Nya 1:5-7 Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. 3Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. 4Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani. 5Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
6Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. 7Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani. 8Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. 9#Mwa 6:11 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za BWANA. 10#Mik 5:6 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari. 11Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala; 12na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa. 13Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, 14#1 Nya 1:12 na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori. 15Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi, 16na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi, 17na Mhivi, na Mwarki, na Msini, 18na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana. 19#Mwa 13:12-15; 15:18-21; Hes 34:2,12; Yos 12:7 Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha. 20Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
21Naye Shemu ambaye ni baba wa wana wote wa Eberi, na ndugu mkubwa wa Yafethi, akazaliwa wana. 22#1 Nya 1:17 Wana wa Shemu ni Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu. 23Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. 24#Mwa 11:12 Arfaksadi akamzaa Sela, Sela akamzaa Eberi. 25#1 Nya 1:19 Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani. 26Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera, 27na Hadoramu, na Uzali, na Dikla, 28na Obali, na Abimaeli, na Seba, 29na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani. 30Makao yao yalikuwa kutoka Mesha kwa njia ya Sefari, mlima wa mashariki. 31Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao. 32#1 Nya 1:4; Mwa 9:19 Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika.
S'ha seleccionat:
Mwanzo 10: SRUVDC
Subratllat
Comparteix
Copia
Vols que els teus subratllats es desin a tots els teus dispositius? Registra't o inicia sessió
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.