Mwanzo 10
10
Wazawa wa Noa#10:1-32 Katika sura hii tuna watu na mataifa makubwa yaliyojulikana kwa Waisraeli wa kale wa wakati wa kukusanywa au kuandikwa kwa habari hizi. Yaonekana kwamba mataifa hayo yamepangwa katika mafungu matatu: wazawa wa Yafethi (aya 2-5), wazawa wa Hamu (aya 6-20) na wa Shemu (aya 21-31). Licha ya kwamba kuyaweka mataifa hayo pamoja kunaonesha tena umoja wa binadamu wote (wote wametokana na Noa) inaonekana pia kwamba mwandishi (au waandishi) wa nasaba hiyo walitaka pia kuwaweka watu wa Israeli katika uhusiano huo na mataifa mengine; nako kuteuliwa kwa Waisraeli ambako kutaelezwa katika sehemu iliyobaki ya Kitabu cha Mwanzo kuwe pia ni njia ya kusema kwamba Mungu atayapatia mataifa yote baraka zake.
1Baada ya gharika, watoto wa Noa, Shemu, Hamu na Yafethi, walipata watoto wa kiume na wa kike. Hii ndiyo orodha ya wazawa wao:
2Watoto wa kiume wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.#10:2 Orodha hii ya wazawa wa Noa inawataja watu na mataifa au makabila ambayo yaliizunguka Bahari ya Mediteranea, yaani kwenye eneo la Mashariki ya Kati ya Kale: watu walioishi upande wa kaskazini wa Bahari ya Mediteranea, walioshi kusini na mashariki ya bahari hiyo, kufikia Afrika ya kaskazini na hata mpaka Mesopotamia. 3Watoto wa kiume wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama. 4Watoto wa kiume wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Dodanimu. 5Hawa ndio asili ya watu walioenea sehemu za pwani, kila watu kwa lugha yao, kwa jamaa zao na kufuata mataifa yao.
6Watoto wa kiume wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani.#10:6-20 Hamu …Kushi, Misri, Puti na Kanaani: Makabila na mataifa yanayotajwa hapa yalifikiriwa kuishi katika eneo kubwa la Mesopotamia, Ashuru, Kanaani mpaka Afrika kaskazini-mashariki (Kushi). Nao Wafilisti waliishi Kaftori jina lingine la kisiwa cha Krete (Amo 9:7). Waamori waliishi katika sehemu za milima za nchi ya Kanaani. 7Watoto wa kiume wa Kushi walikuwa Seba, Hawila, Sabta, Raama na Sabteka. Watoto wa kiume wa Raama walikuwa Sheba na Dedani. 8Kushi alikuwa baba yake Nimrodi ambaye alikuwa shujaa wa kwanza duniani. 9Alikuwa mwindaji shujaa mbele ya Mwenyezi-Mungu, ndiyo maana kuna msemo usemao, “Kama Nimrodi mwindaji shujaa mbele ya Mwenyezi-Mungu.” 10Miji ya kwanza ya utawala wake ilikuwa Babuloni, Ereki na Akadi, katika nchi ya Shinari.#10:10 Shinari: Rejea Mwa 11:2. 11Kutoka huko, Nimrodi alikwenda Ashuru, akajenga miji ya Ninewi, Rehoboth-iri, Kala na 12Reseni ulioko kati ya Ninewi na mji mkubwa wa Kala.
13Misri alikuwa babu wa Waludi, Waanamu, Walehabi, Wanaftuhi, 14Wapathrusi, Wakasluhi (ambao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.
15Kanaani alikuwa babu yake Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, 16na pia babu yao Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 17Wahivi, Waarki, Wasini, 18Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Baadaye watu wa jamii mbalimbali za Kanaani walitawanyika, 19hata eneo la nchi yao likawa toka Sidoni kuelekea kusini, hadi Gerari mpaka Gaza, na kuelekea mashariki hadi Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu hadi Lasha. 20Hao ndio wazawa wa Hamu kadiri ya makabila yao, lugha zao, nchi zao na mataifa yao.
21Shemu,#10:21 Shemu: Ingawa huyu alikuwa mtoto wa kiume wa kwanza wa Noa hapa anatajwa mwisho kusudi mwandishi aendelee na simulizi la Waebrania (au Waisraeli) ambao wanatajwa kama wazawa wake. mkubwa wa Yafethi, alikuwa baba yao Waebrania wote. 22Watoto wa kiume wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.#10:22 Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu: “Elamu” ni jina la awali la Ashuru na “Aramu” nalo lilikuwa jina la awali la “Siria”. 23Watoto wa kiume wa Aramu walikuwa Usi, Huli, Getheri na Mashi. 24Arfaksadi alimzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. 25Eberi alikuwa na watoto wa kiume wawili: wa kwanza akamwita Pelegi kwa sababu wakati huo watu duniani waligawanyika,#10:25 Watu duniani waligawanyika: Katika Kiebrania kuna mchezo wa maneno: jina “Pelegi” Kiebrania linafanana na neno lenye maana ya “waligawanyika” Kiebrania. Mara kwa mara majina yanayotajwa katika Biblia huwa yana maana fulani, desturi ambayo ni kawaida hata katika mataifa yetu. na wa pili akamwita Yoktani. 26Yoktani alikuwa baba wa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 27Hadoramu, Uzali, Dikla, 28Obali, Abimaeli, Sheba,#10:28 Sheba: Labda eneo hili lilikuwa sehemu ya Afrika au Arabia kusini. Malkia wa Sheba alimtembelea mfalme Solomoni wa Israeli (1Fal 10:1-13). Na “Ofiri” ilikuwa eneo au mahali muhimu ambapo dhahabu ilipatikana (taz 1Fal 9:28; 10:11) na eneo hilo pia linafikiriwa kuwa katika Afrika au Arabia ya kusini. 29Ofiri, Hawila na Yobabu. Hao wote walikuwa watoto wa Yoktani. 30Nchi walimokaa ilienea toka Mesha mpaka Sefari katika nyanda za juu za mashariki. 31Hao ndio wazawa wa Shemu, kadiri ya makabila yao, lugha zao, nchi zao na mataifa yao.
32Hao ndio jamaa za watoto wa Noa, kadiri ya vizazi vyao na mataifa yao. Kutokana nao mataifa yote yalienea duniani baada ya gharika.
S'ha seleccionat:
Mwanzo 10: BHNTLK
Subratllat
Comparteix
Copia
Vols que els teus subratllats es desin a tots els teus dispositius? Registra't o inicia sessió
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993