Mathayo 23

23
Yesu Awakosoa Viongozi wa Kidini
(Mk 12:38-40; Lk 11:37-52; 20:45-47)
1Kisha Yesu akazungumza na watu pamoja na wafuasi wake, akasema, 2“Walimu wa sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kuwaambia Sheria ya Musa inasema nini. 3Hivyo mnapaswa kuwatii. Fanyeni kila wanachowaambia. Lakini maisha yao sio mfano mzuri wa kuufuata. Hawatendi wale wanayofundisha. 4Hutengeneza orodha ndefu ya kanuni na kujaribu kuwalazimisha watu kuzifuata. Lakini sheria hizi ni kama mizigo mizito ambayo watu hawawezi kuibeba, na viongozi hawa hawatazirahisisha kupunguza mzigo kwa watu.
5Wao wanatenda mambo mema tu ili waonwe na watu wengine. Hufanya visanduku vidogo vya Maandiko#23:5 visanduku vidogo vya Maandiko Visanduku vidogo vya ngozi vyenye Maandiko manne muhimu. Baadhi ya Wayahudi walivifunga visanduku hivi kwenye vipaji vya nyuso zao na mkono wa kushoto kuonesha kumpenda au uaminifu wao kwa Mungu na Neno lake. Mafarisayo wengi walitengeneza visanduku hivi vikubwa kuliko vya wengine kuonesha kuwa wao ni watu wa dini kuliko watu wengine. wanavyovaa kuwa vikubwa zaidi. Hufanya mashada ya urembo#23:5 mashada ya urembo Urembo uliotengenezwa kwa nyuzi za sufu au manyoya ya kondoo zinazotambaa mpaka chini kutoka pembe nne za vazi la kusalia au vazi la maombi lililovaliwa na Wayahudi. Urembo huu ulipaswa kuwa ukumbusho wa amri za Mungu (tazama Hes 15:38-41). kwenye mavazi yao ya nje kuwa marefu zaidi ili waonwe na watu. 6Watu hawa wanapenda kukaa sehemu za heshima kwenye sherehe na kwenye viti muhimu zaidi katika masinagogi. 7Wanapenda kuitwa ‘Mwalimu’ Na kusalimiwa kwa heshima na watu kwenye masoko.
8Ninyi nyote ni ndugu, dada na kaka kwa sababu mnaye mwalimu mmoja tu. Hivyo msikubali kuitwa ‘Mwalimu’. 9Nanyi msimwite mtu yeyote duniani ‘Baba’, maana mnaye Baba mmoja tu, naye yuko mbinguni. 10Msikubali kuitwa ‘Mwalimu’, kwa sababu mnaye Mwalimu mmoja tu, naye ni Masihi. 11Kila atakayetumika kama mtumishi ndiyo mkuu zaidi kati yenu. 12Wanaojifanya kuwa bora kuliko wengine watanyenyekezwa kwa lazima. Lakini watu wanaojinyenyekeza wenyewe watafanywa kuwa wakuu.
13Ole wenu#23:13 Ole wenu Ama Itakuwa vibaya kwenu enyi walimu wa sheria na Mafarisayo. walimu wa sheria nanyi Mafarisayo! Ninyi ni wanafiki! Mnawafungia watu njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu, kwa kuwa ninyi wenyewe hamwingii na mnawazuia wale wanaojaribu kuingia. 14#23:14 Nakala zingine za Kiyunani zimeongeza mstari wa 14: “Ole wenu walimu wa sheria nanyi Mafarisayo. Ninyi ni wanafiki. Mnawadanganya wajane na kuchukua nyumba zao. Kisha mnafanya maombi marefu ili watu wawaone. Mtapata adhabu mbaya zaidi.” Tazama Mk 12:40; Lk 20:47.
15Ole wenu walimu wa sheria nanyi Mafarisayo! Ninyi ni wanafiki. Mnasafiri kuvuka bahari na nchi nyingine ili kumtafuta mtu mmoja atakayefuata njia zenu. Mnapompata mtu huyo, mnamfanya astahili maradufu kwenda Jehanamu kama ninyi mlivyo!
16Ole wenu walimu wa sheria nanyi Mafarisayo! Mnawaongoza watu lakini ninyi wenyewe ni wasiyeona. Mnasema, ‘Mtu yeyote akiweka kiapo au nadhiri kwa jina la Hekalu, haimaanishi kitu. Lakini yeyote atakayeweka kiapo kwa kutumia dhahabu iliyo Hekaluni lazima atimize nadhiri au kiapo hicho.’ 17Ninyi ni wasiyeona mlio wajinga! Hamwoni kuwa Hekalu ni kuu kuliko dhahabu iliyo ndani yake? Hekalu ndilo huifanya dhahabu kuwa takatifu!
18Na mnasema, ‘Mtu yeyote akitumia madhabahu kuweka nadhiri au kiapo, haina maana yeyote. Lakini kila anayetumia sadaka iliyo kwenye madhabahu na kuapa au kuweka nadhiri, lazima atimize nadhiri au kiapo hicho.’ 19Ninyi ni wasiyeona! Hamwoni kuwa madhabahu ni kuu kuliko sadaka yoyote iliyo juu yake? Madhabahu ndiyo inaifanya sadaka kuwa takatifu! 20Kila anayeitumia madhabahu kuapa au kuweka nadhiri ni dhahiri anatumia madhabahu na kila kitu kilicho juu yake. 21Na kila anayetumia Hekalu kuapa au kuweka nadhiri kwa hakika analitumia Hekalu na Mungu, anayeishi ndani humo. 22Kila anayetumia mbingu kuapa au kuweka nadhiri anakitumia kiti cha enzi cha Mungu na yule aketiye juu yake.
23Ole wenu walimu wa sheria nanyi Mafarisayo! Ninyi ni wanafiki! Mnampa Mungu sehemu ya kumi ya chakula mnachopata,#23:23 Mnampa Mungu … mnachopata Sheria ya Musa iliwataka Waisraeli kumtolea Mungu sehemu ya kumi ya mazao yao (tazama Law 27:30-32; Kum 26:12). hata mnanaa, binzari na jira.#23:23 mnanaa, binzari na jira Haya ni mazao yaliyotolewa malipo ya fungu la kumi. Lakini sheria ya Musa halikujumuisha mazao madogo kama haya yaliyotajwa hapa. Bali Mafarisayo walikuwa wanatoa zaidi ili kuwa na uhakika kuwa hawavunji Sheria. Lakini hamtii mambo ya muhimu katika mafundisho ya sheria; kuishi kwa haki, kuwa wenye huruma, na kuwa waaminifu. Haya ndiyo mambo mnayopaswa kufanya. Na mwendelee pia kufanya mambo hayo mengine. 24Mnawaongoza watu lakini ninyi wenyewe ni wasiyeona!#23:24 lakini ninyi wenyewe ni wasiyeona Hii ina maana kuwa “Mnajishughulisha kwa mambo madogo sana lakini mnatenda dhambi kubwa.” Ninyi ni kama mtu anayemtoa nzi katika kinywa chake na kisha anammeza ngamia!
25Ole wenu walimu wa sheria nanyi Mafarisayo! Ninyi ni wanafiki! Mnaosha vikombe na sahani zenu kwa nje. Lakini ndani yake vimejaa vitu mlivyopata kwa kuwadang'anya wengine na kujifurahisha ninyi wenyewe. 26Mafarisayo, ninyi ni wasiyeona! Safisheni kwanza vikombe kwa ndani ili viwe safi. Ndipo vikombe hivyo vitakuwa safi hata kwa nje.
27Ole wenu walimu wa sheria na ninyi Mafarisayo! Ninyi ni wanafiki! Ninyi ni kama makaburi yaliyopakwa rangi nyeupe, lakini ndani yake yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu. 28Ndivyo ilivyo hata kwenu. Watu wanawatazama na kudhani kuwa ninyi ni wenye haki, lakini mmejaa unafiki na uovu ndani yenu.
29Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo! Ninyi ni wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii, na kuyaheshimu makaburi ya wenye haki waliouawa. 30Na mnasema, ‘Ikiwa tungeishi nyakati za mababu zetu, tusingewasaidia kuwaua manabii hawa.’ 31Hivyo mnathibitisha kuwa ninyi ni uzao wa wale waliowaua manabii. 32Na mtaimalizia dhambi waliyoianza mababu zenu!
33Enyi nyoka! Ninyi mlio wa uzao wa nyoka wenye sumu kali! Hamtaikwepa adhabu. Mtahukumiwa na kutupwa Jehanamu! 34Hivyo ninawaambia: Ninawatuma manabii na walimu wenye hekima na wanaojua Maandiko. Lakini mtawaua, mtawatundika baadhi yao kwenye misalaba na kuwapiga wengine katika masinagogi yenu. Mtawafukuza kutoka katika mji mmoja hadi mwingine.
35Hivyo mtakuwa na hatia kutokana vifo vyote vya watu wema wote waliouawa duniani. Mtakuwa na hatia kwa kumwua mtu wa haki Habili, na mtakuwa na hatia kwa kuuawa kwa Zakaria#23:35 Habili, Zakaria Katika Agano la Kale la Kiebrania, hawa ni watu wa kwanza na wa mwisho kuuawa. Tazama Mwa 4:8-11 na 2 Nya 24:20-25. mwana wa Barakia mliyemwua kati ya Hekalu na madhabahu. Mtakuwa na hatia ya kuwaua watu wote wema walioishi kati ya wakati wa Habili mpaka wakati wa Zakaria. 36Niaminini ninapowaambia kuwa mambo haya yote yatawapata ninyi watu mnaoishi sasa.
Yesu Awaonya Watu wa Yerusalemu
(Lk 13:34-35)
37Ee Yerusalemu, Yerusalemu! Unayewaua manabii. Unawapiga kwa mawe wale ambao Mungu amewatuma kwako. Mara nyingi nimetaka kuwasaidia watu wako. Nimetaka kuwakusanya watu wako kama kuku anavyowakusanya vifaranga wake chini ya mbawa zake. Lakini hukuniruhusu kufanya hivyo. 38Sasa Hekalu lako litaachwa ukiwa kabisa. 39Ninakwambia, hautaniona tena mpaka wakati utakaposema, ‘Karibu! Mungu ambariki yeye anayekuja katika jina la Bwana.’”#Zab 118:26

S'ha seleccionat:

Mathayo 23: TKU

Subratllat

Comparteix

Copia

None

Vols que els teus subratllats es desin a tots els teus dispositius? Registra't o inicia sessió