Mathayo 5
5
Mafundisho ya Yesu Mlimani
(Lk 6:20-23)
1Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda kwenye kilima na kukaa chini. Wanafunzi wake walimjia Yesu. 2Kisha Yesu akaanza kuwafundisha watu kwa akasema:
3“Heri#5:3 Heri Maana yake ni baraka kuu. kwa walio maskini na wenye kujua kwamba wanamhitaji Mungu.#5:3 maskini … wanamhitaji Mungu Kwa maana ya kawaida, “maskini wa roho”, ama wenye uhitaji wa kiroho.
Kwa kuwa ufalme wa Mungu ni wao.
4Heri kwa wenye huzuni sasa.
Kwa kuwa watafarijiwa na Mungu.
5Heri kwa walio wapole.
Kwa kuwa watairithi nchi.#5:5 watairithi nchi Wataurithi ulimwengu ujao yaani ufalme wa Mungu unaokuja.
6Heri kwa wenye kiu na njaa ya kutenda haki.#5:6 wenye kiu na njaa ya kutenda haki Kwa maana ya kawaida, “wenye njaa na kiu ya kutenda haki zaidi ya kitu kingine chochote”.
Kwa kuwa Mungu ataikidhi kiu na njaa yao.
7Heri kwa wanaowahurumia wengine.
Kwa kuwa watahurumiwa pia.
8Heri kwa wenye moyo safi,#5:8 wenye moyo safi Au wenye mawazo safi ama wenye kukusudia mema moyoni, ama wenye nia njema moyoni.
Kwa kuwa watamwona Mungu.
9Heri kwa wanaotafuta amani.#5:9 wanaotafuta amani Au “wapatanishi wa watu waliofarakana”.
Kwa kuwa wataitwa watoto wa Mungu.
10Heri kwa wanaoteswa kwa sababu ya kutenda haki.
Kwa kuwa ufalme wa Mungu ni wao.
11Heri kwenu ninyi pale watu watakapowatukana na kuwatesa. Watakapodanganya na akasema kila neno baya juu yenu kwa kuwa mnanifuata mimi. 12Furahini na kushangilia kwa sababu thawabu kuu inawasubiri mbinguni. Furahini kwa kuwa ninyi ni kama manabii walioishi zamani. Watu waliwatendea wao mambo mabaya kama haya pia.
Ninyi ni Kama Chumvi na Nuru
(Mk 9:50; 4:21; Lk 14:34-35; 8:16)
13Mnahitajika kama chumvi inavyohitajiwa na wale waliopo duniani. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezi kufanywa chumvi tena. Haina manufaa yoyote isipokuwa hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14Ninyi ni nuru inayong'aa ili ulimwengu uweze kuiona. Ni kama mji uliojengwa juu ya kilima unavyoonekana wazi. 15Watu hawawashi taa na kuificha kwenye chungu. Bali huiweka kwenye kinara cha taa ili nuru iangaze kwa kila mtu. 16Kwa namna hiyo hiyo mnapaswa kuwa nuru kwa ajili ya watu wengine. Hivyo ishini katika namna ambayo watakapoyaona matendo yenu mema, watamtukuza Baba yenu wa mbinguni.
Yesu Afundisha Kuhusu Sheria ya Musa
17Msifikiri kwamba nimekuja kuiharibu Sheria ya Musa au mafundisho ya manabii. Sikuja kuyaharibu mafundisho yao bali kuyakamilisha. 18Ninawahakikishia kuwa hakuna jambo litakaloondolewa katika sheria mpaka mbingu na nchi zitakapopita. Hakuna hata herufi ndogo ama nukta katika Sheria ya Musa itakayotoweka mpaka hapo itakapotimizwa.
19Kila mtu anapaswa kutii kila amri iliyo katika sheria, hata ile isiyoonekana kuwa ya muhimu. Kila atakayevunja mojawapo ya amri hizi ndogo na kuwafundisha wengine kuzivunja atahesabiwa kuwa ni mdogo sana katika ufalme wa Mungu. Lakini kila anayeitii na kuwafundisha wengine kuitii sheria atakuwa mkuu katika ufalme wa Mungu. 20Ninawambia, ni lazima muitii sheria ya Mungu kwa kiwango bora kuliko kile cha walimu wa sheria na Mafarisayo. La sivyo, hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.
Yesu Afundisha Kuhusu Hasira
21Mmesikia kuwa hapo kale baba zetu waliambiwa, ‘Usimwue yeyote. Na yeyote atakayeua atahukumiwa.’#Kut 20:13; Kum 5:17 22Lakini ninawaambia, msimkasirikie mtu yeyote kwa sababu mkifanya hivyo mtahukumiwa. Na mkimtukana mtu yeyote, vivyo hivyo mtahukumiwa na baraza kuu. Na ukimwita mtu kuwa ni mjinga, utakuwa katika hatari ya kutupwa kwenye moto wa Jehanamu.
23Unapokwenda kutoa sadaka yako madhabahuni na ukakumbuka kuwa kuna mtu ana jambo dhidi yako. 24Unapaswa kuiacha sadaka yako kwenye madhabahu na uende kupatana na mtu huyo. Ukiisha patana naye ndipo urudi na kuitoa sadaka hiyo.
25Akiwepo mtu anayetaka kukushtaki, patana naye haraka. Jitahidi kufanya hivyo kabla ya kufika mahakamani, hata kama bado mpo njiani. Usipofanya hivyo anaweza kukupeleka kwa hakimu. Na hakimu atakupeleka kwa walinzi watakaokufunga gerezani. 26Ninakuhakikishia kuwa hautatoka huko mpaka umelipa kila kitu unachodaiwa.
Yesu Afundisha Kuhusu Uzinzi
27Mmesikia ilisemwa kuwa, ‘Usizini’.#Kut 20:14; Kum 5:18 28Lakini ninawaambia kuwa mwanaume akimwangalia mwanamke na akamtamani, amekwisha kuzini naye katika akili yake. 29Jicho la kuume likikufanya utende dhambi, liondoe na ulitupe. Ni bora kupoteza sehemu moja ya mwili wako kuliko mwili wako wote ukatupwa Jehanamu. 30Na mkono wako wa kuume ukikufanya utende dhambi, uukate na kuutupa. Ni bora kupoteza sehemu moja ya mwili wako kuliko mwili wako wote kutupwa Jehanamu.
Yesu Afundisha Kuhusu Talaka
(Mt 19:9; Mk 10:11-12; Lk 16:18)
31Ilisemwa pia kuwa, ‘Kila anayemtaliki mkewe ni lazima ampe hati ya talaka.’#Kum 24:1 32Lakini ninawaambia kuwa, kila atakayemtaliki mkewe kutokana na sababu isiyohusiana na uzinzi, anamfanya mke wake kuwa mzinzi. Na kila atakayemwoa mwanamke aliyetalikiwa, atakuwa anazini.
Yesu Afundisha Kuhusu Kiapo
33Pia, mmesikia hapo kale baba zetu waliambiwa, ‘Unaweka kiapo, usishindwe kutimiza kile ulichoapa kufanya. Timiza kiapo ulichoweka mbele za Bwana.’ 34Lakini ninawaambia mnapoweka ahadi, msiape kwa jina la mbingu, kwa sababu mbingu ni kiti cha enzi cha Mungu. 35Na usiape kwa jina la dunia kwa sababu, dunia ni mahali pa kuweka miguu yake. Wala msiape kwa jina la mji wa Yerusalemu, kwa sababu nao ni mali yake Mungu, aliye Mfalme Mkuu. 36Pia usiape kwa jina la kichwa chako kana kwamba ni uthibitisho kuwa utatimiza kiapo, kwa sababu huwezi kuufanya hata unywele mmoja wa kichwa chako kuwa mweusi au mweupe. 37Sema ‘ndiyo’ tu kama una maana ya ndiyo na ‘hapana’ tu kama una maana ya hapana. Ukisema zaidi ya hivyo, utakuwa unatoa kwa Yule Mwovu.
Yesu Afundisha Kuhusu Kisasi
(Lk 6:29-30)
38Mmesikia ilisemwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’#Kut 21:24; Law 24:20; Kum 19:21 39Lakini ninawaambia msishindane na yeyote anayetaka kuwadhuru. Mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na la kushoto pia. 40Mtu akitaka kukushitaki ili akunyang'anye shati, mpe na koti pia. 41Askari akikulazimisha kwenda naye maili moja,#5:41 maili moja Kama kilomita moja na nusu. nenda maili mbili pamoja naye. 42Mpe kila anayekuomba, usimkatalie anayetaka kuazima kitu kwako.
Wapende Adui Zako
(Lk 6:27-28,32-36)
43Mmesikia ilisemwa kuwa, ‘Wapende rafiki zako#Law 19:18 na wachukie adui zako.’ 44Lakini ninawaambia wapendeni adui zenu na waombeeni wale wanaowatendea vibaya. 45Mkifanya hivi mtakuwa watoto halisi walio kama Baba yenu wa mbinguni. Yeye huwaangazia jua watu wote, bila kujali ikiwa ni wema au wabaya. Huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46Ikiwa mnawapenda wale wanaowapenda ninyi, kwa nini mpate thawabu toka kwa Mungu? Hata watoza ushuru hufanya hivyo. 47Na ikiwa mnakuwa wema kwa rafiki zenu tu, ninyi si bora kuliko wengine. Hata watu wasiomjua Mungu ni wakarimu kwa rafiki zao pia. 48Ninalosema ni kuwa, mkue hata kufikia upendo kamili#5:48 kamili Neno “kamilifu”, hapa lina maana “imeendelezwa kwa ukamilifu”, na inaelezea aina ya upendo ambao watoto wanaweza kujifunza kutoka kwa baba. alionao baba yenu wa Mbinguni kwa watu wote.
S'ha seleccionat:
Mathayo 5: TKU
Subratllat
Comparteix
Copia
Vols que els teus subratllats es desin a tots els teus dispositius? Registra't o inicia sessió
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Toleo la Awali
© 2017 Bible League International

: