Matendo UTANGULIZI
UTANGULIZI
Kitabu cha Matendo ya Mitume ni sehemu ya pili ya maandishi ya Luka. Katika ile sehemu ya kwanza, yaani Injili iliyoandikwa na Luka, mwandishi aliamua kutupatia tu habari zile zilizohusu maisha ya Yesu hapa duniani. Walakini baada ya Yesu Kristo kupaa mbinguni, kuwako kwake kati ya wafuasi wake kunachukua hali nyingine: Hawamwoni tena kwa macho, ila wanaamini yupo kati yao, yaani katika jumuiya ya waumini wake au kanisa.
Kitabu cha Matendo ya Mitume chaelezea basi kuweko kwa Yesu Kristo miongoni mwa watu wake kwa njia ya Roho wake ambaye ndiye mwenye kuwapa uhai na nguvu ya kumhubiri Kristo na kuwafanya watu wengi wawe wafuasi wake.
Kwa hiyo shabaha au lengo la kitabu hiki ni kuonesha jinsi wafuasi wake Yesu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu, walivyoeneza Habari Njema ya Yesu Kristo huko Yerusalemu, Yudea, Samaria, na hata miisho ya dunia (1:8). Hiki, aghalabu ni kitabu cha historia ya mwanzo wa Ukristo.
Kitabu chenyewe chaweza kugawanywa katika sehemu kubwa tatu:
Sura 1:1–8:3 Mwanzo wa jumuiya ya Wakristo huko Yerusalemu baada ya kupaa kwake Yesu mbinguni.
Sura 8:4–12:25 Kuenea kwa Habari Njema katika sehemu nyingine za nchi.
Sura 13:1–28:31 Kuenea kwa Habari Njema katika nchi zilizopakana na Bahari ya Mediteranea hadi Roma, mji mkuu wa dola la Waroma.
Matukio yanayoelezwa katika kitabu hiki yanafungua mpango maalumu ambao Kanisa la nyakati zote litafuata: Kutangaza Habari Njema ya Yesu Kristo kwa binadamu wote wa lugha, taifa, rangi, mila zote, mpaka miisho ya dunia. Tena kazi hiyo inafanyika siyo kwa nguvu za mtu bali kwa nguvu na msukumo wa Roho wake Kristo ambaye anaongoza kazi yake.
S'ha seleccionat:
Matendo UTANGULIZI: BHND
Subratllat
Comparteix
Copia
Vols que els teus subratllats es desin a tots els teus dispositius? Registra't o inicia sessió
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Més informació sobre Biblia Habari Njema