1
Mwanzo 22:14
Neno
NEN
Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire. Hadi leo inasemekana, “Katika mlima wa BWANA itapatikana.”
Porovnat
Zkoumat Mwanzo 22:14
2
Mwanzo 22:2
Kisha Mungu akamwambia, “Mchukue mwanao, mwana wako wa pekee umpendaye, Isaka, uende nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima nitakaokuambia.”
Zkoumat Mwanzo 22:2
3
Mwanzo 22:12
Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”
Zkoumat Mwanzo 22:12
4
Mwanzo 22:8
Abrahamu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.
Zkoumat Mwanzo 22:8
5
Mwanzo 22:17-18
Hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga wa pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao, na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.”
Zkoumat Mwanzo 22:17-18
6
Mwanzo 22:1
Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!” Abrahamu akamjibu, “Mimi hapa.”
Zkoumat Mwanzo 22:1
7
Mwanzo 22:11
Lakini malaika wa BWANA akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!” Akajibu, “Mimi hapa.”
Zkoumat Mwanzo 22:11
8
Mwanzo 22:15-16
Basi malaika wa BWANA akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili, akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee
Zkoumat Mwanzo 22:15-16
9
Mwanzo 22:9
Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaka mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni.
Zkoumat Mwanzo 22:9