Logo YouVersion
Ikona vyhledávání

Mwanzo 22

22
Kujua uthabiti wa Abrahamu
1 Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!”
Abrahamu akamjibu, “Mimi hapa.”
2 Kisha Mungu akamwambia, “Mchukue mwanao, mwana wako wa pekee umpendaye, Isaka, uende nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima nitakaokuambia.”
3 Abrahamu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaka mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia. 4Siku ya tatu Abrahamu akainua macho, akapaona mahali pale kwa mbali. 5Akawaambia watumishi wake, “Kaeni hapa pamoja na punda, wakati mimi na kijana tunaenda kule. Tutaabudu na kisha tutawarudia.”
6 Abrahamu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaka mwanawe, naye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja, 7Isaka akamwambia Abrahamu baba yake, “Baba yangu!”
Abrahamu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.”
Isaka akasema, “Moto na kuni zipo. Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”
8 Abrahamu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.
9 Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaka mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni. 10Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe. 11Lakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!”
Akajibu, “Mimi hapa.”
12 Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”
13 Abrahamu akainua macho, akaona nyuma yake kondoo dume akiwa amenaswa pembe zake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire.#22:14 maana yake Bwana atapata Hadi leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.”
15Basi malaika wa Bwana akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili, 16akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema Bwana, kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee: 17Hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga wa pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao, 18na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.”
19Ndipo Abrahamu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wote, wakaenda hadi Beer-Sheba. Naye Abrahamu akaishi huko Beer-Sheba.
Wana wa Nahori
20 Baada ya muda, Abrahamu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto; amemzalia ndugu yako Nahori wana:
21Usi mzaliwa wake wa kwanza, Buzi nduguye,
Kemueli (baba wa Aramu),
22Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli.”
23 Bethueli akamzaa Rebeka.
Milka alimzalia Nahori nduguye Abrahamu hao wana wanane.
24Suria wake Nahori aliyeitwa Reuma pia alizaa wana:
Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka.

Právě zvoleno:

Mwanzo 22: NEN

Zvýraznění

Kopírovat

Porovnat

Sdílet

None

Chceš mít své zvýrazněné verše uložené na všech zařízeních? Zaregistruj se nebo se přihlas