Logo YouVersion
Ikona vyhledávání

Yohana MT. 13

13
1HATTA kabla ya siku kuu ya Pasaka, Yesu akijua ya kuwa saa yake imefika atakayotoka katika ulimwengu huu kwenda kwa Baba, akiwa aliwapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapeuda ukomo wa upendo. 2Hatta wakati wa chakula cha jioni, Shetani alipokwisha kumtia Yuda, mwana wa Simon Iskariote, moyo wa kumsaliti, 3bassi Yesu akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu, na anakwenda kwa Mungu, 4akaondoka chakulani, akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifungia. 5Kiisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu yao, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifungia. 6Bassi akafika kwa Simon Petro. Huyu akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? 7Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyayo mimi, wewe huyafahamu sasa; lakini utayajua baadae. 8Petro akamwambia. Hutanitawadha miguu milele. Yesu akamwambia, Nisipokutawadha, huna fungu pamoja nami. 9Simon Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hatta mikono yangu na kichwa changu pia. 10Yesu akamwambia, Aliyekwisha kuoga hana haja illa ya kunawa miguu, hali yu safi mwili wote; na ninyi m safi, lakini si nyote. 11Maana alimjua atakaemsaliti, ndio maana alisema, Hamwi safi nyote. 12Bassi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Mmeelewa niliyowatendea. 13Ninyi mwaniita Mwalimu, na Bwana; na mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. 14Bassi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa ninyi nanyi kutawadhana miguu. 15Kwa kuwa nimewapeni mfano illi hayo niliyowatendea ninyi, na ninyi mtende yayo hayo. 16Amin, amin, nawaambieni, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake: wala mtume si mkuu kuliko yeye aiiyempeleka. 17Mkiyajua hayo, m kheri mkiyatenda. 18Sisemi khabari za ninyi nyote: nawajua niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aulae mkate pamoja nami ameinua kisigino chake juu yangu. 19Tangu sasa nawaambieni kabla hayajatukia, illi yatakapotukia, mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye. 20Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeae ye yote nimpelekae, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenipeleka. 21Alipokwisha kusema haya, Yesu akafadhaika rohoni, akashuhudu, akinena, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti. 22Wanafunzi wakatazamana, wakiona mashaka, ni nani anaemtaja, 23Palikuwako mmoja wa wanafunzi wake, amemwegamia Yesu kifua chake, ambae Yesu alimpenda. 24Bassi Simon Petro akampungia mkono huyo, amwulize, Ni nani anaemtaja? 25Bassi yeye akimwegamia Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani? 26Bassi Yesu akajibu, Ni mtu yule nitakaemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akampa Yuda, mwana wa Simon Iskariote.
27Na baada ya lile tonge, Shetani akamwingia. Bassi Yesu akamwambia, Uyatendayo, yatende upesi. 28Wala hapana mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu hatta akamwambia hivi. 29Maana wengine, kwa kuwa Yuda aliuchukua mfuko, walidhani ya kuwa Yesu alimwambia, Nunua tunavyovihitaji kwa siku kuu; au kwamba awape maskini kitu. 30Bassi huyu, akiisha kupokea lile tonge, akatoka marra hiyo; na ulikuwa usiku hapo alipotoka.
31Bassi huyo alipokwisha kutoka, Yesu akanena, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, na Mungu ametukuzwa ndani yake: 32Mungu akiwa ametukuzwa ndani yake, Mungu nae atamtukuza ndani ya nafsi yake; na marra atamtukuza. 33Enyi watoto wachanga, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta: na kama nilivyowaambia Wayahudi, ya kama, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja: sasa nawaambia na ninyi. 34Amri mpya nawapeni, mpendane; kama vile nilivyowapenda ninyi, na ninyi mpendane vivyo hivyo. 35Hivi watu wote watajua ya kuwa m wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. 36Simon Petro akamwambia, Bwana, unakwenda wapi? Yesu akamjibu, Niendako, huwezi kunifuata sasa; lakini utanifuata baadae. 37Petro akamwambia, Bwana, kwa nini nisiweze kukufuata sasa? Nitauweka uzima wangu kwa ajili yako. 38Yesu akamjibu, Je! uzima wako utauweka kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jogoo hatawika hatta utakapokuwa umenikana marra tatu.

Právě zvoleno:

Yohana MT. 13: SWZZB1921

Zvýraznění

Sdílet

Kopírovat

None

Chceš mít své zvýrazněné verše uložené na všech zařízeních? Zaregistruj se nebo se přihlas